Habari za Punde

Balozi Seif akagua ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Askari Polisi kisiwani Pemba

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea Ripoti ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Askari Polisi wa Mikoa Miwili ya Pemba kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Msaidizi Kamishna wa Polisi  Said Omar Dadi.
 Muonekano wa moja ya Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi wa Mikoa Miwili ya Pemba zinazojengwa katika Mtaa wa Pujini Chake chake Pemba.
Balozi Seif  akimpongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba na Wapiganaji wake kwa hatua waliyofikia ya ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Wapiganaji hao.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uamuzi wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania wa kujitafutia Nyumba za Makaazi ya Askari wake  ni jambo la msingi litakalosaidia kurejesha Heshima ya Jeshi hilo.
Alisema kitendo cha Askari kuishi Mitaani pamoja na Raia kwa kiasi kikubwa kinapunguza uwajibikaji wa walinzi hao kunakosababishwa na ukaribu unaochangia kushindwa kumchukulia hatua jirani au Jamaa anayekuwa naye pamoja Askari husika kwa muda mwingi.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipofganya ziara fupi ya kuukagua mradi wa ujenzi wa Nyuumba za Makaazi za Jeshi la Polisi zinazojengwa katika eneo la Kambi ya Jeshi hilo iliyopo katika Mtaa wa Mfikiwa Chake Chake Kisiwani Pemba.
Alisema raia anapofanya makosa katika mazingira anayoishi pamoja na Askari Polisi, mlinzi huyo anakuwa mzito kumchukulia hatua za kisheria Raia huyo jambo ambalo hupunguza nidhamu ya kazi ya Ulinzi.
Balozi Seif  aliupongeza Uongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa hatua uliofikia wa kufikia maamuzi ya kuwatafutia stara wapiganaji wake ili kuwapunguzi hofu wanapokuwa Mitaani hasa pale wanapowachukulia hatua za kisheria Wananchi wanaoishi nao Mitaani.
“ Mimi mwenyewe wakati wote ninapokutana naViongozi wenu wa ngazi ya Juu kama IGP nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa Jeshi la Polisi kuwa na nyumba zao za Makaazi ili kupunguza maisha ya uraiani yanayochangia uzoroteshji wa majukumu ya Jeshi hilo”. Alisisitiza Balozi Seif.
Alisema Seikali zote mbili Nchini Tanzania ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar zilikuwa na wakati mgumu wa kufikiria kulitafutia ufumbuzi tatizo la Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi Nchini lililokuwa kero kwa muda mrefu.
Mapema akitoa Taarifa ya ujenzi wa Mradi huo wa Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Polisi Mikoa Miwilio Kisiwani Pemba Kamanda wa Polisi Mkoa Kusini Pemba  Kamishna Msaidizi wa Polisi Said Omar Dadi alisema mradi huo ulianzishwa maalum kwa lengo la kupunguza ifunyu wa Nyumba za Makaazi ya Askari.
Kamishna Msaidia wa Polisi Said alimueleza Balozi Seif  kwamba  mradi huo unaendelea vyema kwa ujenzi wa Nyumba Sita Awamu ya kwanza zitakazokuwa na uwezo wa kuishi Familia 24.
Kamanda huo wa Polisi Mkoa Kusini Pemba kwa niaba ya Askari wa Jeshi hilo Kjisiwani Pemba amewashukuru na kuwapongeza Viongozi wa Serikalik zote mbili Nchini Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono uendelezaji wa ujenzi wa Nyumba hizo muhimu kwa Jeshi la Polisi.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdullah alisema Uongozi wa Mkoa huo pamoja na Wananchi wataendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuona Mradi huo unafanikiwa kama ulivyokusudiwa.
Mh. Hemed alisema ushirikiano huo umejitokeza pale mradi huo ulipokumbwa na changamoto ya upatikanaji wa rasilmali ya Mchanga ambayo Mkoa ukatumia busara zake katika kuitafutia dawa Changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.