Habari za Punde

CDEA, COSOTA Waendesha Kongamano la Kusaidia Wabunifu Kupata Mitaji.











Na. Mwandishi Wetu.
Kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji  (2nd Mashariki Creative Economy Impact Investment Conference) lenye kauli  mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’ llilokuwa la siku mbili Oktoba 11-12, 2018 limemalizika  huku wadau na Wabunifu mbalimbali kutoka Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki  wakipata kujadili changamoto katika sekta hiyo.
Awali akifungua kongamano hilo Oktoba 11,2018 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi  ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhe. Charles Mwijage  amesema Sekta ya ubunifu ina umuhimu wake hivyo wadau wanatakiwa kuwaangalia kwa jicho la pili katika kuwasaidia wabunifu  ili kuendeleza mitaji yao  kwani ina umuhimu wake kwa sababu ndio inaleta biashara, huduma, bidhaa na teknolojia mpya.
Amefafanua kuwa, ni  jinsi gani ubunifu unaongeza ufanisi kwa namna ya kipekee  na ubunifu  huo unavyofanya kazi na kuachana na kazi za mazoea.
“Wabunifu wetu wanamawazo mengi.   Kwa mfano watumiaji wa Electroniki Media (digital) labda anaandaa program ya watoto  namna ya kusoma ‘online’  huo ni ubunifu.  Sasa changamoto  taasisi za kifedha wao wanaangalia  zaidi namna ada yao inavyoweza kurudi, lakini wazo au ubunifu huo aliofanya huyo msanii je Benki pengine wasiuone
..biashara inaweza kulipa kwa hiyo ni moja ya changamoto wanayokutana nayo wabunifu wengi nchini na kwingine kote hapa Duniani” ameeleza Aritiside Mbwasi.
Kwa hatua hiyo amebainisha kuwa, sekta hiyo inaumuhimu wake na mijadala ya kongamano hilo itakuja na hitimisho la kuwasaidia wabunifu namna ya kupata mitaji.
Aidha, amesema moja ya pendekezo pengine ambalo wadau hao wanatakiwa kuangalia ni namna ya kushirikiana na wawekezaji  wengine ambao tayari wao wana fedha  ama mtaji ili kuingia ubia wa kuungana kwenye shea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya Afrika Mashariki  la  (Culture and Development  East Africa - CDEA),  Bi Ayeta Anne Wangusa amesema kongamano hilo lililoandaliwa kwa kushirikiano na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na kuwezeshwa  kwa msaada wa wadau wa OSIEA na British Council,  wanategemea wadau washiriki watakuja na majibu juu ya wabunifu kupata mikopo kutoka kwa wadau wenye mitaji.
Naye Mtaalmu na mtafiti wa kimaitafa  wa viwanda vya ubunifu,  Dkt. Keith Nurse, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Dunia la Uchumi, kwenye  tasisi ya Sir Arthur Lewis Institute for Social and Economic Studies ndani ya chuo kikuu cha West Indies, amesema kuwa wabunifu wengi Duniani wamekuwa na matamanio ya maendeleo makubwa lichaya kukosa fursa tarajiwa kwa wakati.
Aidha, Dkt. Nurse ametoa mifano jinisi haki ubunifu imetumika kama dhamana ya kukopesha wabunifu kutoka nchi zilizoendelea na nchi  zinazoendelea.
Kongamano limeendesha mijadala mbalimbali kutoka kwa watalum wa sheria, fedha, haki miliki na haki ubunifu, kutoka Afrika Mashariki.
Aidha, wadau mbalimbali wanaoshughulikia masuala ya haki miliki kutoka serekalini na  mashirika kama CISAC, wajumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wizara zinahohusika na haki miliki toka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki,
Benki ya Maendeleo  Afrika Mashariki, Benki za kiuchuni, wawekezaji wa Afrika mashariki, mawakili wa haki miliki, vyombo vya hakimiliki vya Afrika Mashariki na wasanii mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wameudhuria kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.