Habari za Punde

Jamii ishajiishwe kupima afya zao na kutambua vichocheo vinavyosababisha kupata maradhi yasiyoambukiza.

Katibu wa Jumuiya ya Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (ZNCDA) Louis  H. Majaliwa  akiwakaribisha Wanahabari walipofika katika Ukumbi wa  Jumuiya hiyo Mpendae, kusikiliza taarifa ya Mradi wanaoutekeleza wa kuwajengea uwezo Wanajamii kuhusu kujikinga na kudhibiti Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar. Kulia ni Meneja wa Mradi huo Haji Khamis Fundi na kushoto ni Omari Abdalla Ali Mfanyakazi wa kitengo cha Maradhi yasiyoambukiza. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
 Haji Khamis Fundi Meneja wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanajamii kuhusu kujikinga na kudhibiti Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar akizungumza na Wanahabari kuhusu utekelezaji wa Mradi huo huko katika Ofisi yao Mpendae Mjini Zanzibar. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanajamii kuhusu kujikinga na kudhibiti Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Haji Khamis Fundi hayupo pichani. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.
Mratibu wa Tamasha la Vyakula vya Asili Makunduchi Moh’d Simba Hassan akichangia namna Vyakula vya asili vinavyosaidia kupunguza Maradhi yasiyoambukiza. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.

Na  Khadija  Khamis – Maelezo  
Viongozi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wametakiwa kuendelea kuishajiisha jamii ili kupima afya zao na kutambua vichocheo vinavyosababisha kupata maradhi yasiyoambukiza.
Maradhi hayo yanaendelea kuhatarisha ustawi wa jamii kutokana na kuzidi kuongezeka kwa kasi nchini.
Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa kuwajengea uwezo wanajamii kuhusu kujikinga na kudhibiti maradhi yasiyoambukiza Zanzibar, Haji Khamis Fundi huko ofisini kwao Mpendae wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema njia za kujikinga na maradhi hayo ni pamoja na Jamii kuwa na  tabia ya kupima afya mara kwa mara na kuepuka kutumia vyakula vyenye mafuta mengi.
Meneja Haji amesema njia nyingine ni pamoja na kufanya mazoezi ya viungo na kutumia vyakula vya asili.
Akielezea kuhusu Mradi huo Meneja huyo amesema lengo la Mradi huo ni kijenga uwezo wa  Muungano wa Jumuiya ya Watu wanaoishi na Maradhi yasiyoambukiza ili iweze kushirikiana na jamii kujikinga na kudhibiti maradhi hayo.
Amesema kupitia Mradhi huo wameweza kutoa huduma za upimaji wa Maradhi mbali mbali ikiwemo Sukari, Macho na Sinikizo la Damu ambapo jumla ya watu 1,125 walifanyiwa vipimo.
Aidha kupitia Mradi huo jumla ya watoto 283 walipatiwa mafunzo ya lishe ikiwemo kupiga mswaki.
Kwa upande wake katibu wa (ZNCDA) Louis H .Majaliwa alisema jumuiya hiyo imeundwa na jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya mbalimbali ikiwemo kisukari , saratani  pamoja na maradhi ya moyo.
Alisema mradi huo wa Muungano wa Jumuiya za Watu Wanaoishi na Maradhi Yasiyoambukiza ni wa mwaka mmoja kuanzia machi 2018 hadi April 2019 ambao umefadhiliwa na Muungano wa Jumuiya  za Watu Wanaoishi na Maradhi Yasioambukiza ya nchini Denmark.
Aidha alisema Mradi huu unatekelezwa Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kwa kushirikiana na maandalizi ya Tamasha la vyakula vya asili Makunduchi pamoja na Kikundi cha mazoezi cha Mtende.
Nae  Mfanyakazi wa kitengo hicho Omar Abdalla Ali alisema kwa wale wananchi ambao wameshapata maradhi hayo waendelee kuyadhibiti kwa kutumia dawa ipasavyo  na kufuata miiko waliokewa .
Alisisistiza kuwa wananchi hao  waendelee kufanya mazoezi ya viungo pamoja na kutumia vyakula vya asili na kupunguza ulaji wa vyakula vya mafuta kwa wingi
 Jumuiya ya wanaoishi na maradhi yasiyoambukiza Zanzibar imeanzishwa mwaka 2013 chini ya sheria ya jumuiya zisizo za kiserikali (Societies Act No 6 ya mwaka 1995) yenye yenya namba ya usajili 2015 .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.