Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Yaadhimishwa Viwanja Vya Mji wa Fumba Zanzibar.

Mgeni rasmin katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akihutubia hafla hiyo ya Maadhimisho Kitaifa imefanyika katika Viwanja vya Mji Mpya Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja na kuhudhuriwa na Wazee kutoka Mikoa Mitatu ya Unguja. 
Katika Maadhimisho hayo Wazee wamepata huduma ya upimaji wa Afya zao na kupatiwa miwani kwa Wazee waliokuwa na matatizo ya kuona.  
Wazee wakiwa katika viwanja vya Mji wa Fumba wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akihutubia wakati wa maadhimisho hayo ya Siku ya Wazee Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba Mosi.Mwaka huu kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mji wa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawakena Watoto Mhe. Maudline Castico akihutubia na kutowa nasaha zake kwa Wananchi na Wazee wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani zilizoadhimishwa Kitaifa katika Viwanja vya Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Nyumba ya Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar baada ya kumalizika hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Kitaifa imefanyika katika viwanja vya Mji Mpya Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.