Habari za Punde

Mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA Kati ya Malindi na Polisi Umeshindwa Kumaliza Dakika 7 za Mchezo huo. Kutokana Kiza na Kuwekwa Kiporo Hadi Keshokutwa Kumaliza Dakika Hizo 7 Katika Dakika za Nyongeza 30 Baada ya Kutoka Sare ya Bila Kufungano.

Mshambuliaji wa Timu ya Polisi akimpita beki wa Timu ya Malindi wakati wa Mchezo wao wa Nusu Fainali ya Michuano Kombe la FA, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungano katika dakika 90 za mchezo huo.

Muamuzi wa mchezo huo na kuongeza dakika 30 katika mchezo huo wa Nusu Fainali ulichezwa katika Uwanja wa Amaan, katika dakika hizo zikimalikida na kiza kiingia katika uwanja huo na kusababisha mchezo kutomalizika zikiwa zimebaki dakika 7 za mchezo huo wa dakika za nyongeza imebidi refali kuahirisha mchezo huo hadi keshokutwa kumalizia dakika hizo 7 za mchezo huo ili kuweza kumpata mshinda na kushiriki mchezo wa Fainali ya Kombe la FA. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.