Fainali ya Kombe la FA Zanzibar itachezwa kesho kati ya Jamhuri dhidi ya KMKM saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
Bingwa wa Kombe hilo atapata nafasi ya kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya JKU utakaochezwa Oktoba 18, 2018 saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Tumezungumza na afisa habari wa ZFA Abubakar Khatib Kisandu na hapa akituelezea maandalizi ya mwisho kuelekea fainali hiyo.
No comments:
Post a Comment