Habari za Punde

TANESCO YAALIKA WAWEKEZAJI WA VIWANDA, YASEMA UMEME UPO WA KUTOSHA NA KUSAZA

 Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda (wakwanza kulia), akimtembeza Naibu Mkurugenzi wa TANESCO (usambazaji) Mhandisi Raymond Seya, (wapili kulia), kujionea maendeleo ya mradi w aumeme wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Oktoba 12, 2018. 

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limesema liko tayari kupokea uwekezaji wa viwanda vya aina zote kwani hivi sasa kuna umeme wa kutosha, bora na wa uhakika. Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (Ugawaji), Mhandisi Raymond Seya, baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa umeme  Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, Ijumaa Oktoba 12, 2018. “Mradi unafikia mwisho sasa, kwasababu mashine zote zimeshafungwa na uwezo wa mashine hizi ni kuzalisha  Megawati 240, tunamalizia mambo madogo madogo kama ujenzi wa barabara na kupaka rangi lakini pia kujenga ofisi za wafanyakazi.” Alifafanua Mhandisi  Seya Tunataka kuwahakikishia wananchi uwekezaji huu mkubwa wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 750 zote zikiwa zimetolewa na serikali umekamilika na tayari umeingizwa kwenye Gridi ya taifa. “Tunapenda kumshukuru sana Mhe. Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufadhili mradi tunawahakikishia sera ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda itatekeelezwa kikamilifu na sisi kama TANESCO tuko tayari kupokea uwekezaji wa viwanda vya aina zote.” Alisema. Alisema, tayari umeme huo umeingizwa kwenye gridi ya taifa na hadi sasa kwa ujumla kuna kiasi cha umeme kwenye gridi ya taifa Megawati 1500 na ukiangalia repoti za matumizi ya umeme kila siku tunakiuwa na ziada ya Megawati 250 hadi 160, Wikiendi inakuwa zaidi kwa sababu matumizi ya umeme yanapungua kwa hivyo yunapoongeza vyanzo hivi vya uzalishaji umeme tuanzidi mkuwa na uwezo wa kuunganisha wateja zaidi na kutoa huduma iliyo bora.” Alisema. Mhandisi Seya pia alitembelea mradi mwingine wa upanuzi wa Kinyerezi I ambapo miundombinu ya kusimika mashine iko tayari na kwamba zoezi la kufunga mashine hizo litaanza wakati wowote luanzia sasa. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda Alisema miradi yote miwili ni miradi ya kimkakati na kwamba wakati mradi wa Kinyerezi II tayari umekamilika, mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, umefikia asilimia 70. “Mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, utakuwa na Megawati 185 ambapo Kinyerezi I yenyewe inazalisha umeme Megawati 150 na hivyo utafanya jumla ya Megawati 335 utakapokamilika Agosti mwakani. “Kwa hiyo miradi yote hii itakapokamilika tunazungumzia jumla ya Megawati 575 zitakuwa zinazalishwa hapa Kinyerezi.” Alifafanua Mhandisi Mmanda. “Sasa hivi kwenye Gridi ya Taifa tunatosheleza mahitaji yote na tuna ziada, kwa hiyo tunachosema kama Shirika la umeme tunao umeme wa mkutosha na wawekezaji waje ili tuweze ili twende na falsafa ya Rais wetu ya kuwa na nchi yenye uchumi wa kati lakini zaidi sana nchi yenye uchumi wa viwanda.” Alsiema. Mhandisi Mmanda alibainisha kuwa Mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I utakamilika Agosti mwakani.

 Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda (wapili kulia), akimpatia maelezo Naibu Mkurugenzi Mtedaji wa TANESCO (usambazaji), Mhandisi Raymond Seya, kuhusu namna mitambo katika chumba cha udhibiti (Control room) inavyofanya kazi
 Meneja Miradi Mwandamizi  TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona, akikagua mitambo kwenye chumba cha udhibiti (Control room) cha Kinyerezi II leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.
 Mhandisi Seya (kushoto), akiteta jambo na Mhandisi Mmanda.
 Naibu Mkurugenzi Mtedaji Shirika la Umeme nchini TANESCO anayeshughulikia usambazaji, Mhandisi Raymond Seya, (katikati), kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, akitembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo leo Ijumaa Oktoba 12, 2018. Kulia ni Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda (kulia) na Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Leila Muhaji,.
 Moja ya mitambo ambayo tayari imewasili ili kutekeleza mradi mwingine wa upanuzi wa Kinyerezi I.
Muonekano wa eneo itakapofungwa mitambo kwenye eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi I hadi kufikia leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.