Habari za Punde

Mgombea Uwakilishi wa Chama Cha AAFP Achukua Fomu ya Kugombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar Katika Uchaguzi Mdogo Unaotarajiwa Kufanyika Tarehe 27/10/2018.

Gari lililomleta Mgombea wa Chama cha AAFP Bi. Amina Juma Abdallah likiwasili katika viwanja vya Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara Zanzibar kwa ajili ya kuchukua Fomu za kuwania nafasi za Uchaguzi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar, baada ya Mwakilishi wa Jimbo hilo kuvuliwa Uongozi na Chama Chake na Jimbo hilo kuwa wazi na kuitishwa Uchaguzi Mdogo kujaza nafasi hiyo. 
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Bi. Amina Juma Abdallah akimsikiliza Msimamisi wa Uchaguzi Jimbo la Jangombe akitowa maelezi jinsi ya ujazaji wa Fomu ya kuwania Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar, 
Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jangombe Zanzibar Bi. Mwanapili Khamis Mohammed akitowa maelezo kwa mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Bi. Amina Juma Abdallah, akiwa na Katibu Mkuu wa AAFP Zanzibar. wakati wa hafla hiyo ya uchukuaji wa Fomu hiyo.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Jangombe Zanzibar Bi. Mwanapili Khamis Mohammed (kulia) akimkabidhi Fomu ya Kugombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Bi. Amina Juma Abdallah, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mjini Maisara Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar Bi. Amina Juma Abdallah, kupitia Chama cha AAFP, asisaini fomu ya uchuaji wa Fomu ya Uwakilishi wa Jimbo la Jangombe Zanzibar. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.