Habari za Punde

Mkutano wa Wafanyakazi wa PBZ Wakati wa Bonaza la Pili Mwaka 2018 Viwanja Vya Kendwa Rocks Nungwi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOWU Bi. Rihi Haji Ali akimkabidhi zawadi ya Vikombe vyenye Nembo ya PBZ na ZAFICOWU, wakati wa mkutano huo wa Wafanyakazi kabla ya kuaza kwa Bonaza la PBZ 2018, katika viwanja vya Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Ameir Hafidh.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Wazanzibar Ndg Juma Ameir Hafidh akionesha Zawadi ya Kikombe aliokabidhiwa na Katibu Mkuu wa ZAFICOWU kwa ajili ya Wafanyakazi wa PBZ wakati wa mkutano huo kati ya Wafanyakazi wa PBZ na Uongozi wa ZAFICOWU, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi, Khadija Shamte na Katibu wa ZAFICOWU Bi. Rihi Haji Ali.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi. Khadija Shamte akizungumza na Wafanyakazi wa PBZ wakati wa mkutano huo wa Wafanyakazi na Uongozi wa ZAFICOWU, kabla ya kuaza Bonaza la PBZ 2018, katika viwanja vya Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOWU Bi. Rihi Haji Ali akizungumza na Wafanyakazi na Uongozi wa PBZ wakati wa mkutano wa Wafanyakazi wa Bonaza katika ukumbi wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. na kutowa nasaha zake kwa Uongozi wa PBZ katika mafao ya Wanachama wake katika PBZ.kulia Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi.Khadija Shamte, Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh na Mwenyekiti wa ZAFICOWU Ndg Mussa Yussuf. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Ameir Hafidh akizungumza na Wafanyakazi wa PBZ katika ukumbi wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaszkazini Unguja wakati wa hafla ya Bonaza la Pili 2018, na kuzungumzia changamoto katika utendaji wa kazi zao za kila siku,kabla ya kuaza kwa Bonaza la Wafanyakazi katika ufukwe wa pwani ya Kendwa Rocks kwa michezo mbalimbali ya kuvuta kamba, kufukuza kuku,mpira wa ufukweni na mchezo wa nage.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh, akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wa PBZ katika ukumbi wa hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja katika hafla ya michezo ya Bonaza la Wafanyakazi katika ufukwe wa pwani ya Nungwi Zanzibar.
Wakurugenzi wa PBZ wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ wakati akizungumza na Wafanyakazi wa PBZ katika hafla ya mchezo wa BONAZA katika ufukwe wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Zanzibar.
Wakurugenzi wa PBZ wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ wakati akizungumza na Wafanyakazi wa PBZ katika hafla ya mchezo wa BONAZA katika ufukwe wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh wakati akizungumza na Wafanyakazi wa PBZ kabla ya kuaza kwa Bonaza la PBZ katika ufukwe wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wafanyakazi wa PBZ wakifuatilia Mkutano huo wakati wa hafla ya Bonaza katika ukumbi wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Afisa Mwandamizi wa PBZ Ndg.Mohammed Khamis akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo na kujianda ni michezo ya Bonaza katika ufukwe wa Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Zanzibar. Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Imetayarishwa na Zanzinews.com.
Othman Mapara.
othmanmaulid@gmail.com.
0777424152.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.