Habari za Punde

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga Awashauri Wasanii Wanaopiga Picha za Utupu Kuacha Tabia Hiyo.

1Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga (katikati) akiwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakiwa wameongozana na   Wakurugenzi pamoja na Wazee wa kabila la Wamwela wakati kutembelea nyumba ya kabila la Mwela katika kijiji cha Makumbusho  kabla ya kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akizungumza na  Athumani Issa wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiwasaidia akina Mama wa kabila la Wamwela  kutwanga nafaka  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akipewa kibuyu chenye  pombe na Halima Abdallah ambacho kimekuwa kikitumiwa na kabila hilo kunywea pombe  wakati alipotembelea nyumba ya kabila la Wamwela katika kijiji cha Makumbusho wakati wa   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii, Mhe. Japhet  Hasunga akiangalia baadhi ya mabaki ya samaki aina ya nguva aliyekutwa amekufa kando kando mwa bahari ya Hindi mkoani Lindi wakati alipotembelea mabanda  kabla ya   kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji hicho  jijini Dar es salaam. 
  1. Baadhi ya vikundi vya ngoma vikitumbuiza wakati wa  kufunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika kijiji cha Makumbusho    jijini Dar es salaam
                              ( Picha na Lusungu Helela)   


NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  amewashauri wasanii wanaopiga picha za utupu waache kupiga picha hizo badala yake watembelee Hifadhi za Taifa ili wakapige picha na simba, twiga chui pamoja na sokwe kwa ili  waweze kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Pia amewataka wasanii wenye nia ya kutaka kutengeneza filamu  katika Hifadhi ya Taifa wawasaliane na Uongozi wa Hifadhi za Taifa au wawasiliane na  yeye mwenyewe moja kwa moja.

Ametoa rai hiyo wakati  akifunga tamasha  la utamaduni wa mtanzania inayowakilishwa na jamii za mkoa wa Lindi lililofanyika kwa muda wa siku nne katika  kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam

Aidha, Ameiasa jamii iitumie mitandao ya kijamii kujipatia elimu badala ya kusambaza picha ambazo ni kinyume cha maadili ya Mtanzania.

Ameongeza kuwa Jamii iwakemee wasanii wenye tabia hiyo badala ya kusubilia Serikali ndo ichukue hatua.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.