Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Aaza Ziara Mkoa wa Kagera.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Bukoba kuanza awamu ya pili ya ziara ya mkoa huo itakayodumu kwa siku nne.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama Ngoma ya kikundi cha Kakau Band wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kuanza awamu ya pili ya ziara ya mkoa huo itakayochukuwa siku nne.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma bango lenye malalamiko ya mmoja wa wananchi wa Bukoba wakati alipowasalimia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuwasili kwa ziara ya siku nne mkoani humo, Oktoba , 2018.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali  Marco Elisha Gaguti na kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

Baadhi ya wafanyabiashara wa  zao la kahawa  wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.