Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Mhe. Kidawa Hamid Saleh, akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza jambo kuhusiana na changamoto zinazotokea katika utendaji wa huduma za kibenki kwa wateja wao.
Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo,
katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki ya watu wa Zanzibar, Mperani Mwenyekiti
wa bodi hiyo, Kidawa Hamid Saleh alisema uimarishaji huo utasaidia kupunguza
changamoto zinazoikabili benki hiyo.
Hata hivyo,
alisema ni vyema kwa wafanyakazi kuongeza bidii katika uwajibikaji na kuendelea kuwa waadilifu ili wafanikishe
malengo yabenki hiyo ambayo aliitaja kuwa tegemeo kwa wananchi.
Aidha,
aliwataka wajumbe hao kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa vile Zanzibar ina
benki nyingi zinazotoa huduma kwa wanachi.
Sambamba na
kuongeza kuwa katika kuhakikisha huduma zinapatikana, watatumia mawakala katika
maeneo mbalimbali kwa lengo la kufikisha huduma karibu kwa wananchi.
Hata hivyo,
Mwenyekiti huyo alihimiza ushirikiano kwani alieleza kuwa ndio msingi ambao
utailetea mafanikio benki hiyo pamoja na kuhakikisha wateja wanapata huduma
bora.
Naye,
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Juma Ameir Hafidh alisema wanampango wa
kuanzisha matawi mapya na kutoa huduma kupitia wakala ili kurahisisha huduma
kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment