Habari za Punde

Balozi Seif mgeni rasmi maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye ulemavu Duniani

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiingia kwenye Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni kuhudhuria  kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani akiwa Mgeni rasmi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.
 Balozi Seif Kulia akimkabidhi Zawadi Bibi Jouaquiline Mohan Mwakilishi wa Shirika la Umojawa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA} kazi kubwa ya usimamizi wa Mpango wa usajili wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza Vijana Walemavu  wasioona Awena na Jamila baada ya kusoma utenzi katika mahadhi yaliyoleta ladha kwenye sherehe hizo.
 Baadhi ya washiriki wa kilele cha maadhimisho ya ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani zilizofanyika hapo Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.
 Baadhi ya Washiriki wa maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye ulemavu Duniani wakiserebuka wakati Kikundi cha Taarab cha Wajela jela kikitoa burdani kwenye Maadhimisho hayo.


 Balozi Seif akimpongeza Bibi Zeyana Ahmed Mlemavu baada ya kusoma Risala kwa ufasaha ya Shirikisho la Watu wenye ulemavu kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani.
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bwana Haidar Hashim Madewea akito salamu za Baraza hilo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani.Wa kwanza Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdulla Hassan Mitawi.
 Baadhi ya Watu wenye ulemavu wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye Kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani kwenye Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania wakifuatilia matukio tofauti yaliyojiri ndani ya Ukumbi huo.
 Balozi Seif akibonyesha kitufe kwenye Kompyuta kuashiria kuzindua Rasmi Mfumo wa kuhifadhi Taarifa za Watu wenye Ulemavu Zanzibar akishuhudiwa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu {UNFPA} Bibi Jouquiline Mohan Kushoto yuake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Znzibar Balozi Seif kuzungumza na Wananchi mbali mbali katika kilelecha siku ya Kimataifa ya Watu wenye ulemavu Duniani.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.