Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Atembelea Kisiwani Pemba Kuangalia Matayarisho ya Maandalizi ya Sherehe za Mapinduzi.

 Kamanda wa Jeshi la ananchi wa Tanzania Meja Khamis akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hatua zitakazochukuliwa na Jeshi siku ya Mkesha wa Tarehe 12 Januari wakati wa upigwaji wa Fash Fash na Mizinga hapo katika Uwanja wa Tibirinzi Chake Chake

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa maelezo ya mfumo utakaotumika wa Kituo cha Waalikwa wa sherehe za Mapinduzi hapo uwanja wa kufurahishia Watoto Tibirinzi watakaoanzia kuelekea  uwanja wa Gombani.
 Balozi Seif na Wajumbe wa Kamati ya Sherehe ya Maadhimisho ya Kitaifa wakiangalia Ukumbi wa Hoteli ya Misali Wesha utaotumiwa kwa kikao cha Watendaji wa SMT na SMZ mara baada ya kumalizika kwa sherehe za Mapinduzi.
Balozi Seif na Ujumbe wake wakiangalia sehemu ya Nje ya Uwanja wa Ndege wa Pemba itakayofanyiwa matengenezo kwa ajili ya kuhudumia Wageni watakaohudhuria sherehe zaMapinduzi Kisiwani Pemba.
 Balozi Seif na Timu yake wakikagua maeneo mbali mbali ya Uwanja wa Ndege zikisemu Sehemu Maalum kwa Wageni Mashuhuri {VIP} na kuridhika na hatua iliyofikiwa.
 Mkurugenzi Biashara na Masoko ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Nd. Juma Saleh alimueleza Balozi Seif hatua zilizofikiwa za matengenezo ya Uwanja huo.
Afisa Mdhamizi Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Usafirishaji Nd. Ahmed Baucha akimthibitishia Balozi Seif kukamilika kwa uwekwaji Lami eneo la nyongeza la maegesho ya Uwanja wa Ndege wa Pemba baada ya kupata Mafuta.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rrais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara Maalum ya kuangalia harakati za Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi Matrukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 katika maeneo tofauti ndani ya Wilaya ya Chake chake Kisiwani Pemba.
Ziara hiyo aliyoambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa aliianzia katika Uwanja wa Michezo wa Tibirinzi unaotarajiwa kutumika kwa sherehe za Fash Fashi katika mkesha wa Maadhimisho ya Sherehe hizo.
Akitoa Taarifa za maandalizi hayo Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ali Salum Ali Matar alisema usafi wa mazingira wa uwanja huo unaendelea kufanywa na Vikosi vya Ulinzi kwa kushirikiana na baadhi ya Wananchi.
Nd. Matar alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba  endapo siku hiyo itazunguukwa na hali ya Mvua  licha ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kanda ya Zanzibar kutabiri hali ya mkawaida kipindi hicho, Kamati ya Maandalizi imependekeza Sherehe hizo kuzihamishia katika Uwnja wa Gombani ya Kale.
Naye Kamanda wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania {ZWTZ} Meja Khamis alisema shughuli ya upigaji Mizinga na Fash fash utafanyika kwa kuzingatia maelekezo ya Uongozi wa Jeshi hilo.
Meja Khamis aliwatoa hofu Wananchi wote kwamba Mizinga itakayotumika katika Mkesha huo haitakuwa na madhara yoyote jambo ambalo Wananchi hao wanaweza kuendelea na harakati zao za kimaisha kama kawaida.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikagua Hosteli ya Achipelago iliyopo Tibirinzi pamoja na Ile ya Misali zilizoteuliwa kuhudumia Viongozi  Mashuhuri wakiwemo wale Wastaafu wa Serikali zote mbili, Mabalozi wa Kigeni waliopo Nchini Tanzania pamoja na Mawaziri wa Serikali zote mbili.
Balozi Seif pia alitembelea Kiwancha cha kufurahishia Watoto kilichoteuliwa kuwa Kituo Kikuu cha Wageni wote watakaohudhuria Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi zitakazofikia kilele chake Tarehe 12 Januari 2019 katika Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake chake Pemba.
Wageni wote watafikia Kituoni hapo kwa kupata chai na baadae kupanda Mabasi Maalum yaliyotayarishwa kuwahudumia kwa mujibu wa Kadi walizopangiwa ili kuondosha usumbufu unaoweza kuepukwa mapema.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimalizia ziara yake kwa kukagua Uwanja wa Ndege wa Chake Chake kujionea hatua ilioyofikiwa ya matengenezo mbali mbali yatayotoa fursa ya kukidhi mahitaji ya Viongozi wataotumia Uwanja huo.
Mkurugenzi Biashara na Masoko ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Nd. Juma Saleh alimueleza Balozi Seif kwamba maeneo yote yaliyomo kwenye ratiba ya matengenezo kwenye Uwanja huo yako katika kiwango cha kumalizia.
Nd. Juma alisema Ukumbi wa Wageni Mashuhuri {VIP} umeshakamilika matengenezo yake ukibakisha ubadilishwaji wa Vikalio, Eneo la Maegesho ya Ndege liko katika hatua ya uwekwaji wa kifusi pamoja na kumalizia Sehemu za Mbele za Jengo la Uwanja huo.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na hatua mbali mbali zilizochukuliwa na matayarisho ya Sherehe hizo na kuwataka Viongozi wa Kamati mbali mbali zilizoteuliwa kusimamia masuala hayo kuhakikisha kwamba kasoro zilizobaki katika mambo yote zinamalizika kwa wakati uliopangwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.