NAIBU Waziri wa
Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi
Atashasta Nditiye akiwasili katika uwanja wa ndenge wa Pemba Airport, kwa ziara
ya kuangalia maeneo ambayo miwasiliano ya simu hayapatikani katika Mkoa wa
Kaskazini Pemba
AFISA Mdhamini Wizara
ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba Hamad Ahmed Baucha, akiutambulisha
ugenzi wa Wizara ya Uchukuzi Mawasiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakati ulipofika kwa mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla,
Katikatiugenzi huo ukiongozwa na Naibu waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Atashasta
Nditiye
MKUU wa Mkoa wa
Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman Abdalla wanne kutoka kushoto, akiwa na Naibu waziri
wa Wizara ya Uchukuzi Mawasiliano ya Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Atashasta
Nditiye wakati wa picha ya pamoja baada ya ujumbe wa naibu huyo kujitambulisha
katika ofisi hiyo ya mkuu wa Mkoa
NAIBU waziri wa
Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Atashasta
Nditiye, akizungumza mara baada ya kukikagua kituo cha Tehama kilichopo katika
Ofisi ya Tawala za Mikoa Machomanne Chake Chake Pemba
MBUNGE wa Viti
maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Maida Hamad Abdalla, akutambulisha ugeni wa
Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ukiongozwa na Naibu waziri wa Wizara hiyo Mhe.Atashasta Nditiye uliofika katika
Shehia ya Kiungoni juu ya Kuangania upatikanaji wa mawasiliano ya simu
NAIBU waziri wa
Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Atashasta
Nditiye, akizungumza na wananchi wa shehia ya Kiungoni Wilaya ya Wete, juu ya
ukosefu wa mawasiliano ya siku katika shehia hiyo, wakati alipofanya ziara ya
kuangalia maeneo ambayo usikivu wake wa mawasiliano mdogo sana
MKURUGENZI wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhandisi Piter Ulanga akizungumza na wananchi wa Shehia ya Kiungoni, baada ya
kusikia kilio cha ukosefu wa usikivu wa mawasiliano ya simu katika shehia hiyo
SHEHA wa shehia ya
Kiungoni Omar Khamis Othman, akizungumza na waandishi wa habari kutoka Vyombo
mbali mbali vya habari, juu ya uwepo wa usikivu mdogo wa mawasiliano ya simu
katika shehia yake
MKUU wa WIlaya ya
Micheweni Bi.Salama Mbarouk Khatib, akizungumza juu ya hali ua usikuvu hafifu ya
mawasiliano ya simu kwa wananchi wa Wilaya ya Micheweni, wakati wa kikao na
Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Atashasta Nditiye, huko katika skuli ya sekondani Wingwi.
Picha na Abdi Suleiman -Pemba.
No comments:
Post a Comment