Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji
Profesa Makame Mbarawa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Maji safi
na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack
Kamwelwe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex
Mubiru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi
mkubwa wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira utakaosaidia jiji la Arusha katika
sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Kimyaki Arumeru mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia maji yanayotoka katika moja ya
visima virefu vilivyopo katika mradi huo mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira
katika jiji la Arusha. Mradi huo utakapokamilika utaweza kuzalisha lita za
ujazo milioni 200 kwa siku tofauti na
sasa ambapo lita za ujazo ni 45 milioni wakati mahitaji ya jiji la Arusha ni
lita za ujazo milioni 90.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Alex Mubiru wakati wa mkutano na wananchi wa
Arumeru jijini Arusha mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arumeru mara baada
ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Maji
safi na usafi wa Mazingira katika jiji la Arusha
Wananchi wa Arumeru wakishangilia
wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli katika kijiji cha Kimnyaki Arumeru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka
katika eneo la mkutano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha Calist
Lazaro mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Arumeru. Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment