Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu
wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa
Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa
Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric pamoja na Waakilishi wa
Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli akihutubia katika hafla ya Utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha Umeme
katika mto Rufuji, Mkataba ambao umesainiwa leo 12 Disemba ,2018 Ikulu Jijini
Dar es Salaam, kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya ujenzi ya Arab Constructor kutoka nchini Misri.
Waziri Mkuu wa Misri
Mustapha Madbouly akiongea katika Hafla
ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa umeme katika mto Rufuji
uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Ujenzi kutoka nchini
Misri(Arab Constructors) Ujenzi
utakaochukua takribani miaka mitatu kukamilika kwake na kuweza kutoa megawati
za umeme 2115.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu wa Misri Mustapha
Madbouly (wa tatu kushoto), Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania
Mama Samia Suluhu Hassan( wa tatu kulia), Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa(wa
pili kushoto) na Spika wa Bunge la Mungano wa Tanzania Job Ndugai (wa pili
kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri na Manaibu Waziri baada ya
Hafla fupi ya utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa mRdi wa umeme wa mto Rufiji,
mkataba uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya ujenzi kutoka
Misri Arab Constructors leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya
pamoja na Wajumbe wa Kamati ya
majadiliano ya Mkataba wa Ujenzi wa
Mradi wa bwawa la umeme mto Rufiji mara
baada ya hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa mradi huo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es
Salaam leo
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mbalimbali mara baada
ya hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa mradi wa umeme wa mto Rufuji uliosainiwa
kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni
ya Ujenzi ya Arab Contructors kutoka
nchini Misri leo 12 Disemba , 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment