Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akitokea Nchini Uingereza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Uingereza leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Nchini Uningereza leo.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,
amerudi nchini leo akitokea Uingereza.
Katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume viongozi mbali mbali wa
Serikali, vyama vya siasa pamoja na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
walimpokea Rais Dk. Shein.
Wakati huo huo, Rais Dk. Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika mazoezi ya viungo kwa wananchi wote yatakayofanyika kisiwani Pemba
ambayo yataanzia Wawi Matrekta hadi uwanja wa Gombani.
Mazoezi
hayo yatafanyika siku ya Jumaane Januari 1, 2019 ikiwa ni miongoni mwa shamra
shamra za miaka 55 ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.
Siku
hiyo hiyo, mnamo majira ya saa kumi za jioni Rais Dk. Shein atafungua skuli ya
Msingi Chimba iliyopo Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Jumaatano
ya tarehe 2 Januari 2019 saa nne za asubuhi Rais Dk. Shein anatarajia kuzindua
vituo vya Uokozi vya KMKM kwa niaba ya Vituo vya Uokozi vya KMKM vya Kiweni na
Nungwi hafla itakayofayika katika Bandari
ya Mkoani Pemba.
Uwanja
wa Michezo wa Mao-Tse Tung uliopo Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja utafunguliwa
na Rais Dk. Shein siku ya Alhamis ya Januari 3, 2019 mnamo majira ya saa kumi
za jioni.
Aidha,
Rais Dk. Shein ataifungua Barabara ya Kijitoupele hadi Fuoni Mambosasa iliyopo
Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi mnamo siku ya Jumaamosi ya
tarehe 5 Januari 2019 mnamo saa nne za asubuhi.
Rais
Dk. Shein ataweka Jiwe la Msingi katika jengo la Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na
Nishati pamoja na ZURA lililopo Maisara, Wilaya ya Mjini Unguja mnamo siku ya
Jumaapili ya Januari 6, 2019.
Jumanne
ya Januari 8, 2019 Rais Dk. Shein anatarajia kufungua Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali iliyopo Maruhubi, Wilaya ya Mjini Unguja.
Pamoja
na hayo, Rais Dk. Shein anatarajiwa kufungua Skuli ya Sekondari ya Bwefum
Wilaya ya Magharibi B Unguja mnamo siku ya Jumaatano ya Januari 9, 2019 ambapo
jioni yake anatarajia kutoa nishani hafla itakayofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Kilele
cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zitafanyika
siku ya Jumaamosi ya Januari 12, 2019 katika uwanja wa Gombani uliopo Chake
Chake Pemba ambapo Rais Dk. Shein atakuwa mgeni rasmi.
Mnamo
majira ya saa mbili za usiku siku hiyo hiyo ya Januari 12, 2019 Rais Dk. Shein
atakuwa Mgeni Rasmi katika Taarab Rasmi ya Kikundi cha Taifa itakayofanyika
katika kiwanja cha Kufurahishia Watoto cha Tibirinzi kiliopo Chake Chake Pemba.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment