Mkurugenzi wa Mifumo ya
Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi, akieleza kuhusu bidhaa mpya
zitakazo wasilishwa kwa wadau wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG) wakati wa
Mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu ambaye ni mgeni rasmi akifungua
mkutano wa wadau wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG) wa uliofanyika katika
ukumbi wa wa Wizara ya Fedha na Mipango (Kambarage) Jijini Dodoma.
Meza kuu ikiongozwa na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (katikati)
wakifuatitia kwa makini maelezo ya wadau wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG),
Jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa
mkutano wa mwaka wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG), wakifuatilia hotuba ya
mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu
(hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu ambaye ni mgeni rasmi akiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa watumiaji wa mfumo wa
ukusanyaji mapato uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Kambarage Jijini Dodoma.
(Picha
na Josephine Majura MoFP Dodoma)
Na.
Josephine Majura na Peter Haule WFM, Dodoma
Serikali imezitaka taasisi
zote ambazo bado hazijajiunga na Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato
ya Serikali (GePG) kuhakikisha wamejiunga na mfumo huo kabla ya Juni 30,
2019.
Agizo hilo limetolewa na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu, kwa niaba
ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James, wakati wa Mkutano wa mwaka wa
wadau wa utumiaji wa mfumo wa GePG Jijini Dodoma.
Dkt. Kazungu, alisema
kuwa hakutokuwa na fedha yoyote ya umma itakayokusanywa nje ya Mfumo
wa GePG, hivyo wakati mwafaka wa kujiunga na kuunganishwa na mfumo huo ni
sasa.
“Napenda kusisitiza kuwa,
ni lazima kutumia mfumo huu kwa kuwa unaongeza ufanisi na uwazi katika
ukusanyaji wa Fedha za Umma na pia utaratibu wa matumizi ya GePG unatoa
fursa ya kuwa na njia nyingi za kulipia na kuwapa walipaji wa huduma za
Serikali utaratibu rafiki wa kufanya malipo”, alieleza Dkt. Kazungu.
Utaratibu wa makusanyo
kabla ya mfumo wa GePG haukua rafiki kwa kuwa ilikuwa ni vigumu kuthibitisha malipo na
pia kuwa na foleni ndefu kwenye Ofisi za Serikali zilizosababishwa na
zoezi la kufanyiwa tathmini ya malipo ya huduma na kuthibitisha malipo.
Alisema ili kukabiliana na
changamoto hizo katika ukusanyaji wa Fedha za Umma, Juni 2017, Serikali
iliifanyia marekebisho Sheria ya Fedha za Umma (PFA) ya mwaka 2001 na kuongeza
kipengele kinachotaka Fedha zote za umma zikusanywe kupitia Mfumo wa Government
e-Payment Gateway (GePG).
Lengo la kuanzishwa kwa
GePG ni kutatua changamoto zilizopo kwenye Mfumo uliokuwepo wa ukusanyanji wa
fedha za umma ili kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na
kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma na pia kupunguza gharama
zinazoambatana na ukusanyaji wa fedha hizo ambapo mfumo huo ulianza kutumiwa
rasmi na taasisi za umma mwezi Julai 2017 baada ya majaribio yake kukamilika.
Alisema kuwa utaratibu GePG
unaenda sambamba na utekelezaji wa maelekezo mengine ya Serikali yanayohusu
makusanyo ikiwemo yale yanayotaka akaunti kuu za makusanyo za taasisi za umma
kuwepo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hivyo ni lazima kuhakikisha akaunti za
Taasisi za ummaa za makusanyo zilizoko Benki Kuu zimewasilishwa kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya fedha na mipango ili ziunganishwe na GePG.
Mpaka sasa takribani
Benki kumi na moja (11) na mitandao sita(6) ya malipo kwa njia ya simu za
kiganjani zimeshaunganishwa na mfumo huo.
Dkt. Kazungu alisema kuwa
ni vyema taasisi za Serikali kuwa na akaunti za makusanyo kwenye benki zaidi ya
moja kati ya benki zilizoungwa na GePG ili kuwarahisishia walipaji wa huduma za
serikali kwa kuwa malipo yote yanayopitia GePG hayatozwi ada za miamala na
benki hizo, hivyo kuongeza akaunti za makusanyo hakutoongeza gharama za miamala
kwa taasisi za umma.
Alibainisha kuwa
kutekelezwa kwa rai hiyo kutaondoa hatari ya taasisi ya umma kukosa huduma ya
malipo endapo benki inayotumiwa itashindwa kutoa huduma kwa sababu mbalimbali
ikiwemo kuvunja makubaliano ya namna ya kuzihudumia akaunti zilizounganishwa
kwenye mfumo wa
Naibu Katibu Mkuu Kazungu
amewataka wajumbe wa mkutano huo kuwa chachu katika kuboresha
utendaji kwa vitendo kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi zinazohusisha
ukusanyaji wa Fedha za Umma katika maeneo yao ya kazi baada ya kumalizika kwa
mkutano huo.
Kwa upande wake Mkurungezi
wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi, alisema kuwa
mfumo huo umekuwa na tija tangu ulipoanzishwa kwa kuwa Serikali kupitia Wizara
ya Fedha inaweza kuona makusanyo yote yanayoingia hivyo kuongeza ufanisi wa
upatikanaji wa mapato, uwajibikaji na uwazi.
Alisema kuwa, jumla ya
Taasisi 326 zimeunganishwa na Mfumo wa GePG na miongoni mwa Taasisi hizo
ni Wakala wa Misitu, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO)
Amezitaja changamoto za
Mfumo huo kuwa ni pamoja na Benki 11 tu ndizo zinazotumia mfumo huo kati ya
Benki zaidi ya 50, hivyo kuleta mkanganyiko kwa wadau wanaotumia mfumo huo.
Mkutano wa wadau wote
wanaotumia Mfumo wa GePG ni wa kwanza kufanyika nchini ukiwa na lengo la
kubaini na kutatua changamoto za mfumo huo tangu ulipoanzishwa.
No comments:
Post a Comment