Na.Paschal
Dotto-Maelezo. Dar es Salaam. 29-1-2019.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewataka Majaji, Wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi wa halmashauri wapya walioapishwa
leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, kufanya kazi kwa kuzingatia masharti ya kazi zao
ili kuweza kutoa haki na kuwatumikia wananchi.
“Nawapongeza sana
Majaji sita mahakama ya Rufani 15 mahakama
kuu , Wakuu wa Wilaya wawili na Wakurugenzi wa halmashauri 10 mulioapishwa
leo kikubwa kafanyeni kazi kwa kuzingatia masharti ya kazi zenu, kwa Majaji
kasimamieni haki ili wananachi waweze kuondokana na dhuluma, lakini kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
kasimamieni mapato nchi inahitaji mapato siyo mkaanze mabishano, uongozi ni
kufanya kazi kwa ushirikiano kwa hiyo sidhani kama nitapata malalamiko”, Rais
Magufuli
Rais Magufuli
aliwasisitiza Majaji sita wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama kuu
kwenda kuchapa kazi kwani Serikali inahitaji wananchi wapate haki inayotakiwa
na itakuwa njia bora kwa wananchi kujua haki zao.
Aidha Rais Magufuli
alisema kuwa kuna sehemu hapa Tanzania ambazo imekuwa na dhuluma kubwa akitolea
mfano Halmashauri ya Mufindi ambako tukio la ubakaji lilifanyika na mtuhumiwa
aliachiwa huru.
“Unapotazamwa na watu
wengi na kupimwa, unapopewa kazi ya kusimamia haki hii ni kazi ngumu sana kwa
sababu ina lawama kubwa kwa mfano niliona kwenye Televisheni wamama
wakilalamika kwa Waziri Mkuu Mtaafu Mzee Pinda kuwa kuna mtuhumiwa mmoja huko Mufindi Iringa alifanya
matukio 11 ya ubakaji lakini akaachiliwa huru, vitu hivi vinawaumiza watanzania
kwa bahati nzuri Mhe, Jaji naye aliiona video hiyo mimi nilipoona nilimuagiza
mzee pinda amwambie Mkuu wa Mkoa amshike huyu mtuhumiwa”, Alisema Rais
Magufuli.
Katika tukio hilo
amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro kulifanyia uchukunguzi
tukio hilo lifanyiwe kazi kwa upande wa polisi huku akitoa maagizo kwa Jaji
Mkuu Prof. Ibrahim Juma kufuatilia mahakama
ya Iringa kuona kama ushahidi unaotolewa unatosha .
Akitoa nasaha kwa
wateule hao, Makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa wilaya zote
mbili Mwanga na Tarime kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi kama
walivyoapa mbele ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Nawapongeza Wakuu wapya
wa Wilaya hizi mbili lakini nawaomba mkazifanyie kazi changamoto zilizoko
katika wilaya zenu, kwa mwanga watu wanapigana ngumi nadhani utaenda
kuyarekebisha haya, lakini kwa Wilaya ya Tarime kuna vishawishi vingi sana vya
rushwa pamoja ya unyayasaji wa kijinsia, Ubakaji na kupigwa kwa wanawake kwa
hiyo kayafanyie kazi haya.”, alisema Makamu wa Rais.
Kwa upande wake
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametoa kongole kwa Rais
Magufuli kwa kuteua majaji sita wa Mahakama ya Rufani na 15 wa Mahakama Kuu
kuwa hatua hiyo itaongeza ufanisi katika utoaji haki nchini.
Aidha katika kuongeza
ufanisi wa kushikiliza mashauri mbalimbali hapa nchini Prof. Kabudi alipenyeza
suala la kuwepo kwa mahakama zinazotembea MOBILE COURT ili kuweza kuwafikia
wananchi kwa urahisi.
“Mhe. Rais nashukuru kwa
kunipa hao 15 wa Mahakama kuu na sita wa Mahakama ya Rufani kwani sasa idadi ya
majaji imeongezeka kutoka majaji 66 mpaka majaji 81 kwa Mahakama kuu baada ya
hawa uliowapisha leo”, Jaji Mkuu Prof. Juma
Akielezea mahitaji ya
majaji katika mahakama ya Tanzania Prof. Juma alisema bado Majaji wanahitajika
ili kukidhi hali ya sasa ya kuwahudumia wananchi, aliongeza kuwa bado kuna
umuhimu wa kuongeza Majaji ikiwezekana wawe na idadi ya majaji 100 mpka 150 kwa
sababu kwa sasa wananchi wamezidi kuzijua haki zao.
Jaji Mkuu alisema mahakama
inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mahakama za mwanzo 12 ambazo
zitazinduliwa hivi karibuni,Miradi 36 ya ujenzi itakayozinduliwa Juni mwaka huu,
pamoja na Mahakama 28 za Wilaya nchini.
No comments:
Post a Comment