Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji cha Umbuji Wametowa Shukrani Kwa Serikali Kuwajengea Kituo cha Afya.

Na.Thabit Madai.
UHABA wa madaktari na udogo wa Kituo cha Afya Umbuji kumetajwa ni

tatizo katika upatikanaji wa afya ndani ya kikiji hicho.

Hayo yameelezwa na wananchi wa kijiji hicho walipokuwa wakizungumza na
waandishi wa habari waliofika kituoni hapo ambapo walisema kuwa
wanashukuru kupata kituo hicho lakini kinakabailiwa na changamoto kubwa hizo mbili.

Walisema kuwa wanaishukuru sana Serikali kujengewa kituo hicho lakinibado kuna haja ya kujengwa kituo chengine zaidi ili wananchi waweze kupata huduma bila ya usumbufu.

“Kituo kipo ila ni cha wajawazito lakini tunashangaa kuona kwamba huduma zote zinatolewa pale na hakijakidhi mahitaji yetu kwa vile kesi ya kituo cha afya hapa Umbuji bado tungalinayo”, alisema Maalim Mrisho.

Alisema kuwa huduma  wanapata lakini hata hao wajawazito bado hawajapata kujifunguwa na ikitokea kujifunguwa anapelekwa mjini lakini pia kituo kidogo na sio malengo , wao walitaka kujengewa kituo kikubwa na cha kisasasa kama ambavyo mwakilishi wao alitaka.

 “Huduma zote tunapata, lakini kituo kidogo na kimeandikwa cha mama wajawazito na watoto lakini matokeo yake huduma zote zinafanyika hapo sasa kile kilio cha kituo cha afya Umbuji bado kipo”,alisema Mrisho.

Mrisho Vuai alisema wanaupongeza   mradi wa kukuza uwajibikaji (PAZA) ambao umesaidia kutoa maoni yao na baadhi ya changamoto zinazowakabili katika shehia zao kusikilizwa na kupatiwa ufumbuzi kupitia Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya kati. 


 Nae Khatib Abdalla Mkaazi wa Umbuji alisema kuwa kadhiya yote hii ambayo wanayo alisema kuwa imesababishwa na Serikali yenyewe kutokana na kwamba tayari mwakilishi alishakuwa tayari kukijenga kituo hicho  lakini walimwambia asijenge na watajenga wenyewe ingawa wamejenga lakini hakikidhi haja.


Alisema kuwa kituo ambacho kipo kimekuwa kikitoa huduma kwa wanawake na wanaume lakini kutokana na udogo wa jengo inafikia hatua unapopatiwa huduma unakuwa katika sehemu ya wazi ambayo wagonjwa wote wanakuwepo hapo.

 “Serikali ndio inayotusumbuwa, na nasema hivyo kwa sababu Mwakilishi wetu Raza alitaka kukijenga lakini aliambiwa asikijenge lakini tunashangaa kuona kituo kilichojengwa ni kidogo sana na pia hakuna siri kutokana na mgonjwa wakati akipewa huduma anakuwa kuna wagonjwa wengine wengi wanasikia na wakati magonjwa mengine ni siri”, alisema.

Hivyo alisema kuwa ipo haja ya kujengewa kituo cha afya na ikiwezekana hata kwa ushiikiano na wananchi ili wawe na kituo chenye staha na eneo kubwa la kufanyia kazi.

“Hivi kweli inasahili mgonjwa anaulizwa mawali na sisi tupo wagonjwa wanawake na wanaume, hakuna siri kwa sababu nayoulizwa yote sisi tunayasikia”, alisema.

Hivyo alisema ipo haja ya kujengewa kituo hicho tena kwa haraka kweli kwa sababu wanakihitaji kituo ambacho kipo hakikidhi haja na pia waongezewe madaktari maana madaktari waliopo ni wanne kuna siku AAwengine wanapata semina anabakia mmoja hapo huduma zinaanza kuzorota.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.