Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Akizungumza na Wanachama wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutembelea Miradi ya Maendeleo  


Na.Abdi Shamnah.Ikulu Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein , akiwa pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, alizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Dimani Kichama, Kamati za Siasa za Mkoa Magharibi, Kamati za siasa za Wilaya pamoja an viongozi mbali mbali wa chama hicho, katika ukumbi wa CCM Mkoa, Amani.
Akizungumna wanachama hao, Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwepo umoja na mshikamano ndani ya chama hicho ili kujenga chama bora kitakachohakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.
Alisema nguvu za chama hicho ni umoja, hivyo akawataka wanachama kuendelea kushikamana  na kuepuka mifarakano na utengano, huku akiwataka wanachama kufuata maadili ya chama hicho katika kushajiisha umoja.
Alisema huu ni wakati ambao umoja unahitajika  zaidi ili kuwa katika mazingira bora kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.
Alisema katiba ya CCM imeweka wazi dhamira ya chams hicho kushinda katika chaguzi zote , ili kuendleea kushika dola na kuongoza Serikali.
Alisema ili kufikia hatua ya ushindi ni lazima CCM iendelee kushika mpini, akiweka bayana kuwa mpini huo utashikwa na watu wenye umoja, wanaozingatia maadili na wasio na tamaa.
Alisema Serikali ya Mapinduzi inayoongozwa na CCM ilianza maadalizi ya uchaguzi huo mara tu baada ya uchaguzi wa marudio wa 2016 kwa kuandaa mpango wa utekelezaji wa Ilani,
Alisema serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa Ilani kwa kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo, ikiwemo sekta za maji, barabara, afya na elimu.
Alisema baadhi ya viongozi ikiwemo Wabunge na Wawakilishi hawana habari kabisa na utekelezaji wa Ilani, hivyo akawataka kuwa imara na kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama hicho.
Aidha, aliwataka kutumia vyema muda uliobaki kwa kutekelza ahadi walizozitowa kwa wapiga kura wao ,
Mapema, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,  Abdalla Juma Sadala alisema Uongozi wa Chama Wilaya Dimani umefanya juhudi kubwa za kuwafikia wnaachama wake hadi ngazi za chini pamoja na kutatuwa changamoto mbali mbali ziilizojiri.
Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza ahadi walizozitoa kwa wapiga kura wao,
Aidha, taarifa ya Chama Wilaya hiyo, imebainisha wanachama 27,272 wameandikishwa Wilayani humo, huku asilimia sita ya wanaachama hao wakiwa tayri wamelipa ada za uanachama zilizofikia zaidi ya shilingi Milioni 2.5


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.