Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Balozi wa Saud Arabi Nchini Tanzania Leo.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkaribisha Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Bwana Mohamed Almalk nyumbani kwake Osterbay Jijini Dar es salaam kwa mazungumzo.
Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar Balozi Seif  akimshawishi Kulia Balozi wa Saudi Nchini Tanzania  kuushauri Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Misaada wa Nchi yake kuzuru Tanzania ili kuja kuona miradi waliyoisaidia na kuifadhili.
Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Bwana Mohamed Almalk akisisitiza umuhimu wa Nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania alipokuwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Osterbay Mjini Dar es salaam.

Saudi Arabia Nchini Tanzania Bwana Mohamed Almalk akishindikizwana mwenyeji wake  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumaliza mazungumzo yao.Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mataifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE} naya nafasi kubwa kwa Wananchi wake kufanya ziara za Kiutalii Nchini Tanzania katika azma ya kuendelea kudumisha Uhusiano wa Kihistoria wa pande hizo.
Alisema Umoja wa Falme za Kiarabu na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni Mataifa yanayokaribia kufanana  katika harakati za Kibiashara, Mila, Silka na Utamaduni ambayo yanapaswa kushirikiana katika maisha za kila Siku.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Bwana Mohamed Almalk hapo Nyumbani Kwake Mtaa wa Osterbey Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam.
Alisema Wageni na Watalii wengi wanaofanya ziara ya kimatembezi Nchini Tanzania vikiwemo Visiwa vya Zanzibar wengi wao kwa kipindi hichi wanatokea Mataifa ya Ulaya.
Balozi Seif  alisema kwa vile Saudi Arabia imeonyesha upendo kwa Zanzibar kutokana na kuiunga mkono kwenye harakati za Maendeleo kupitia Sekta za Afya, Kilimo, Bara bara pamoja na Mafunzo ya muda mfupi na Mrefu alimuomba Balozi huyo kuushauri Uongozi wa Mfuko wa Misaada ya Maendeleo wa Saudi Arabia {SAUD FUND} kutenga muda maalum kwa kuitembelea miradi iliyounga mkono nguvu zake.
“ Ingependeza kuona kwamba Uongozi wa Saud Fund unakuja Zanzibar kuikagua Miradi iliyoifadhili pamoja na ile iliyoiongezea nguvu za Uwezeshaji Kifedha”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuishukuru Saudi Arabia Kupitia Mfuko wake huo wa Kimataifa  wa Misaada kwa jitihada inazochukuwa ambazo kwa kiasi kikubwa zimeleta Ukombozi Mkubwa kwa Wananchi walio wengi Visiwani Zanzibar.
Mapema Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Bwana Mohamed Al malk alisema Wananchi wa Mataifa ya Falme za Kiarabu {UAE} wamekuwa wakifuatilia matukio mbali mbali yanayoendelea Nchini Tanzania.
Bwana Mohamed alisema ufuatiliaji huo umewawezesha kutambua fursa za uwekezaji zilizopo Nchini Tanzania hasa katika Sekta ya Utalii, Biashara pamoja na Mawasiliano.
Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba atatumia taaluma yake ya Kidiplomasia kuyashawishi Makampuni na Taasisi za Nchi yake kufungua Milango ya Uwekezaji Nchini Tanzania.
Alisema ushawishi huo pia aliahidi kuuwelekeza kwa kuuomba Uongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa Misaada ya Maendeleo wa Saudi Arabia {Saud Fund} kutembelea Zanzibar kama ombi la Balozi Seif alivyolitoa ili kuangalia hatua za maendeleo zilizofikiwa kupitia nguvu na misaada ya Mfuko huo.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo nyumbani kwake Mtaa wa Osterbay Mjini Dar es salaam.
Katika mazungumao yao Viongozi hao waligusia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Cuba na Zanzibar na Tanzania kwa Jumla uliolenga zaidi katika Sekta za Uwekezaji za Afya, Kilimo pamoja na Elimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.