Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Balozi wa Cuba Nchini Tanzania.

Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tnaznia Profesa Lucas Domingo kati kati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Osterbay Mjini Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Kulia akitilia mkazo umuhimu wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Jamuhuri ya Cuba wakati alipokuwa akizungumza na Balozi wa Nchi hiyo Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo.

Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis. OMPR. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Profesa Lucas Domingo nyumbani kwake Mtaa wa Osterbay Mjini Dar es salaam.
Katika mazungumao yao Viongozi hao waligusia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Cuba na Zanzibar na Tanzania kwa Jumla uliolenga zaidi katika Sekta za Uwekezaji za Afya, Kilimo pamoja na Elimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.