Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAZISHI YA MTOTO WA WAZIRI KIGWANGALLA

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akifariji Waziri wa Maliasi nac Utalii Tannzania Mhe.Dkt. Hamis Kigwangalla, kwa kufiwa nac Mtoto wake.alipofika kuhudhuria msiba Kijiji cha Puge Nzega.  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole  JR Hamisi Kigwangalla kufuatia kifo cha mdogo wake Zul, kulia ni Baba wa Marehemu Zul, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla muda mfupi kabla ya mazishi yaliofanyika Puge wilayani Nzega mkoa wa Tabora.TABORA. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan  ameongoza  shughuli za  mazishi  ya  Zulqarinain mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi Kigwangalla  yaliyofanyika leo Ijumaa Februari 22, 2019 saa kumi jioni katika kijiji cha Puge,  Nzega vijijini jimboni kwa Waziri Kigwangalla.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na   viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri Wabunge pamoja  na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Marehemu Zul alifikwa na mauti  jana majira ya saa nne asubuhi   JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE katika hospitali ya taifa ya Muhimbili  alikokuwa   amelazwa   akiwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

#R.I.P Zul.
Inna lillahi wainna illaihi rajiuun

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.