Habari za Punde

Malezi tunayowapa hata watoto wetu lazima yawe na balance otherwise tunaweza tukawa na watoto kama maua ya Kijana engineer changamoto ndogo tu chali kwasababu ya possessions zetu tunafikiri kuwajali sana na kuwadekeza ndiyo malezi sahihi.*

ASSALAM ALEYKUM!
Majirani wawili wote walikuwa wamepanda maua mazuri pembeni mwa nyumba zao, jirani mmoja alikuwa kijana mmoja Engineer na jirani mwingine alikuwa Mzee Mstaafu.

Kijana Engineer yeye alikuwa anatunza maua yake vizuri sana kwa kuyamwagilia maji vizuri, aliweka mbolea, aliweka madawa ya kuua wadudu, alipalilia vizuri maua yake na maua yake yalipendeza na kuleta mwonekano mzuri sana.

Mzee Mstaafu yeye alikuwa anamwagilia kwa nadra sana, hakuweza kuweka mbolea za kutosha pia, hakuwahi kabisa hata kupulizia madawa ya wadudu kwenye maua yake. Na maua yake yalionekana kuwa si mazuri ukilinganisha na ya jirani kwani maua ya jirani yalikuwa Leafy, super green and luxuarant.

Siku mmoja mvua kubwa ilinyesha maua ya kijana engineer yote yalingolewa na mvua kubwa wakati Maua ya mzee mstaafu yakiwa salama hayajasombwa na mvua. Kijana engineer alishangaa sana maua yangu yenye afya nzuri yamesombwa na mvua ya huyu Mzee yamebaki hiki ni kitu gani.

Kijana Engineer alimwuliza kwa nini Maua yangu yamebebwa na mvua wakati yangu yalikuwa mazuri kuliko yako,  Mzee Mstaafu akajibu Maua yangu sikuyapa Maji ya kutosha kwahiyo kuna kipindi ilibidi mizizi yake iende chini zaidi ilikupata maji ya kutosha wakati maua yako yalipata kila kitu so mizizi haikuwa imezama sana chini ndiyo maana imekuwa rahisi kubebwa na mvua.

*Unaweza ukawa hupati unachokihitaji leo kwenye maisha yako kumbe kitu hicho kinakuandaa kuwa mtu imara zaidi kesho ukikutana na changamoto utaweza kushinda bila hata kujua kumbe mapungufu ya jana ni nguvu ya kesho. Usilie na hali ya sasa bali inakuandaa kuwa mwenye kusimama kesho. Malezi tunayowapa hata watoto wetu lazima yawe na balance otherwise tunaweza tukawa na watoto kama maua ya Kijana engineer changamoto ndogo tu chali kwasababu ya possessions zetu tunafikiri kuwajali sana na kuwadekeza ndiyo malezi sahihi.*

*Siku njema wana wa Mungu tuzidi kudumu katika sala. Kesho yetu ni njema sana*

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.