Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Aendelea na Ziara Yake Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Edward K. Mulumba (kulia) wa Wizara ya Maji  yanayohusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Shinyanga (KASHWASA).
Jengo la Madarasa ya Chuo cha Ualimu SHYCOM ambalo Makamu wa Rais alitembelea na kutaka kujua kwa nini ujenzi wake umesimama. Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa haamini macho yake kuona uchafu uliokithiri mara baada ya kutembelea jiko la kupikia chakula cha wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Taleck (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho John Nandi. 
Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM Happyness Kasuku akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) changamoto ya maktaba ya kusomea ambayo ni ndogo na ina vitabu vichache.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akkizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu.
Wanafunzi Nchambi Nsile (kulia) anayesoma darasa la 7 akiwa amempakata mwenzake Nyazobe Sembe darasa la 4 wa Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wa kumsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo. Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga.
 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.