Habari za Punde

Mkutano wa siku moja juu ya mradi wa afya kamilifu wafanyika kisiwani Pemba

 MRATIB wa Tume ya Ukimwi Kisiwani Pemba Nassor Ali Abdalla, akifungua mkutano wa siku moja kwa waandishi wa habari, juu ya mradi wa afya kamilifu unaoendeshwa na amref Health Africa kanda ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano kutoka tume ya ukimwi Zanzibar, Saadat Sihaba Iddi, akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba,  juu ya uwepo wa mradi wa afya kamilifu unaoendeshwa na Amref Health Africa Kanda ya Zanzibar .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MRATIB wa huduma za kuzuia Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto  kutoka ZCP, Hamida Omar Bungalah, akiwasilisha mada ya juu ya hali halisi ya ushiriki wa kinamama wanaoishi na VVU kwenda kiliniki na watoto wao .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 mratibu wa Mradi wa Afya Kamilifu kutoka  Amref Health Africa kanda ya Zanzibar, Dr Mohamed Hassan akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa waandishi wa habari Kisiwani Pemba, wakati wa kuutambulisha rasmi mradi huo .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
BAADHI ya waandishi wa habari wanaotumia blog wakijadiliana kazi za kufanya wakati wa utekelezaji wa mradi wa afya Kamilifu  unaoendeshwa na Amref Health Africa Kanda ya Zanzibar .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.