Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Akiendelea na Ziara Yake Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba 24-2-2019.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mgodo Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kushoto Mhe. Riziki Pembe Juma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri wakielekea katika jengo la Madarasa ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, na kulia Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Omar Othman.

Jengo Jipya la Madarasa la Skuli ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza kla Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, wakimsikiliza Mwanafunzi wa Skuli ya Mchanga Mdogo akitowa maelezo wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Jengi Jipya la Madarasa la Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba. 
Baadhi ya Meza na Viti vilivyoagizwa kutoa Nje kwa Matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar tayari hatua za mwazo vimeshawasili na kusambazwa katika majengo ya Skuli za Sekondari Unguja na Pemba katika maskuli kwa matumizi ya Wanafunzi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia moja ya meza katika jengo la Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo baada ya kuyafungua Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Maji Ardhi, Nishati na Nyumba Mhe.Salama About Talib, wakiwa katrika moja ya madarasa hayo likiwa na meza na viti vipya  
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, wakiimba Wimbo wa Sisi Sote Tumegomboka, wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza na Wananchi na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba, kutembelea Miradi ya Maendeleo.
Wanafunzi wa Skuli za Sekondari na Msingi Kijiji cha Mchanga Mdogo Kisiwani Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.