Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Atembelea Eneo la Uchimbaji wa Mchanga Finya Selemu Wilaya ya Micheweni Pemba Akiwa katika Ziara Yake leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bi, Maryam Juma Mabodi, akitowa maelezo ya uchimbaji wa mchanga katika eneo la Selemu Finya Wilaya ya Micheweni Pemba akiwa katika ziara yake leo. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, alipata fursa ya kutemebelea maeneo ya Selemu Finya na Shumba Viamboni ambayo yametengwa maalum kwa shughuli za uchimbaji wa mchanga, na hivyo kutoa miongozo juu ya uchimbaji wa rasilima li hiyo.

Hatua ya Dk. Shein inafuatia rasilimali hiyo kupunguwa kwa kiwango kikubwa, hususan katika kisiwa cha Unguja hivyo kulazimika kutoa miongozo ili kuinusuru rasilimali hiyo isije kumalizika katika kisiwa hicho.

Alisema kuna haja ya kuwepo umakini katika rasilimali ya mchanga kisiwani humo, ili iweze kutumika vyema na kwa kipindi kirefu kijacho.

Aidha, katika majumuisho ya ziara yake, Dk. Shein alizungumza na Viongozi na Wanachama wa chama cha Mapinduzi Wilaya Micheweni na kusistiza haja ya kuendeleza umoja na mshikamano, kwa kigezo kuwa ndio chachu ya ushindi wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema viongozi wa Chama na serikali wanawajibu wakufanyakazi kwa mashgirikiano kwa kuzingatia kuwa serikali ilioko madarakani ya Chama cha Mapinduzi, ambapo pia hatua hiyo itawawezesha kutatua kero mbali mbali za wananchi zinazowakabili.

Dk. Shein alisisitiza haja ya viongozi na wanachama wa CCM kuendelea kuwa na umoja na kubainisha kuwa hatua hiyo ndio chachu ya ushindi wa chama hicho sambamba na kuwataka kuepuka kutengeneza migogoro.

Dk.Alisema ameridhishwa na taarifa mbili za utekelezaji za Wilaya hizo zilizowasilishwa kwake ikiwemo ile ya chama pamoja na serikali.

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Bi.Salama Mbarouk alisema alisema katika kipindi cha mwaka 2017/18 hali ya usalama ya Wilaya hiyo imekuwa ya kuridhisha, hali iliyowafanya wananchi kutekeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila vikwazo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.