Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. Aaza Ziara Yake kwa Uzinduzi wa Barabara ya Mkanyageni Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa Kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Barabara ya Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba leo.kushoto Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.Mhe. Sira Ubwa Mwamboya. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Mama Mwanamwema Shein na kulia Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr. Sira Ubwa Mwamboya, wakisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la Barabara ya Mkayageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Mikoa Miwili ya Pemba Kusini na Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri, wakiwa katika viwanja vya Mkanyageni wakati wa hafla ya Uzinduzi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara Mpya iliojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akisoma taarifa ya kiufundi ya ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, baada ya kufunguliwa barabara hiyo leo.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara ya kiwango cha lami katika Kijiji cha Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba, kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kuhutubia katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Barabara. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba,wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Barabara iliojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba,wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Barabara iliojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Mkanyageni hadi Kangani Wilaya ya Mkoani Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.