Habari za Punde

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dk,Hemed Mohamed Al-dhawiyan mara baada ya kuwasili Forodhani kwa ziara maalum ya kuangalia majengo mbalimbali ikiwa pamoja na lililokuwa Jumba la Watoto Forodhan,Makaburi ya Wafalme, Baitul-Ajaib,Ngome kongwe,Makumbusho ya Kasri ,Palace Museum na Nyumba ya moto kwa ajili ya kufanya Tathmini ya matengenezo makubwa ya majengo hayo Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo wapili kulia akimfahamisha jambo Mwenyekiti wa Taifa wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dk,Hemed Mohamed Al-dhawiyan wakati wakilitembelea lililokuwa Jumba la Watoto Forodhan katika ziara maalum ya kuangalia na kufanya Tathmini ya matengenezo makubwa ya majengo hayo Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Dk,Amina Ameir Issa akitoa maelezo kuhusiana naJumba la Ngome Kongwe kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dk,Hemed Mohamed Al-dhawiyan na ujumbe wake wakati wakilitembelea  Jumba hilo katika ziara maalum ya kuangalia na kufanya Tathmini ya matengenezo makubwa ya majengo hayo Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Dk,Amina Ameir Issa akitoa maelezo kuhusiana naJumba la Ngome Kongwe sehemu ya Uchoraji kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dk,Hemed Mohamed Al-dhawiyan na ujumbe wake wakati wakilitembelea Jumba hilo katika ziara maalum ya kuangalia na kufanya Tathmini ya matengenezo makubwa ya majengo hayo Zanzibar.
Jumba la Baitul Ajaib linalotaka kufanyiwa matengenezo makubwa pamoja na majengo mengine yaliokuwepo Forodhani mjini Zanzibar.
Balozi mdogo wa Oman aliekuwepo Zanzibar Dk Ahmad Hamuod Al-Habsi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara ya Ujumbe wa Oman ulioongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dk,Hemed Mohamed Al-dhawiyan ili kutembelea na kufanya Tathmini ya matengenezo makubwa ya majengo hayo Zanzibar.


Picha na Yussuf  Simai - Maelezo ,Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.