JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
|
||||
![]() |
||||
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mtangazaji Mahiri wa Clouds
Media Group, Bw. Ephraim Samson Kibonde kilichotokea jana Jijini Mwanza.
“Msiba
huu ni pigo kubwa kwetu wanatasnia wa
habari nchini, tupo pamoja na wenzetu wa Clouds Media Group katika kipindi
hiki kigumu cha majonzi" amesema Dkt. Mwakyembe.
Enzi
za uhai wake Marehemu Kibonde alikuwa Mtangazaji wa Redio ya Clouds Fm katika
kipindi cha Jahazi, pia alijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo
uandaaji wa vipindi vya kuelimisha Umma
katika masuala ya Makazi na Afya.
Dkt.
Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, uongozi
na wafanyakazi wote wa Clouds Media Group pamoja na wadau wa habari nchini.
Imetolewa na

Lorietha
Laurence
Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
08/03/2019
No comments:
Post a Comment