Habari za Punde

Mkutano wa Viongozi wa CCM wa Mikoa na Wilaya Unguja Kupokelea Ilani Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi akikifunga Kikao cha Viongozi wa CCM wa Mikoa na Wilaya cha kupokea Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Serikali kutoka Mwaka 2015 – 2018 kilichofanyika hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Mjini Zanzibar. 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi akikifunga Kikao cha Viongozi wa CCM wa Mikoa na Wilaya cha kupokea Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Serikali kutoka Mwaka 2015 – 2018 kilichofanyika hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao hicho wakichangia Mda hiyo na kuipongeza Serikali kwa jitihada zake za kutekelzwa kwa mafanikio Ilani ya CCM.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Serikali ina wajibu wa kutoa Taarifa kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi  jinsi inavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 - 2020 iliyopata ridhaa ya Wananchi walio wengi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi alisema hayo wakati akikifunga Kikao cha Viongozi wa CCM wa Mikoa na Wilaya cha kupokea Utekelezaji wa Ilani ya CCM kutoka Mwaka 2015 – 2018 kilichofanyika hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwanduzi Mjini Zanzibar.
Nd. Abdulla Mitawi alisema utaratibu ulioanzishwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa kuwapatia Wananchi Taarifa za Utekelezaji wa Ilani kupitia Viongozi na Chama utasaidia kushusha Taarifa hizo kwa Wananchi ili waelewe wanachofanyiwa na Serkali yao.
Amewaomba Viongozi hao kuyaeleza yale yote yanayofanywa na Serikali chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Naye  Mkurugenzi Utaribu wa Shughuli za Serikali SMT na SMZ kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Khalid Bakari Hamrani akiwasilisha utekezaji huo wa Ilani ya CCM alisema Serikali inayoongozwa na Dr. Shein imejitahidi kuimarisha Uchumi katika azma ya kustawisha Wananchi wa Taifa hili.
Nd. Khalid alitolea mfano uimarikaji wa Uchumi huo unaoonekana wazi katika Sekta za  Miundombinu, Miamala ya Kibenki, Afya. Elimu, Kilimo pamoja na Mawasiliano.
Kwa upande wake mshiriki wa Kikao hicho ambae pia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Nd. Suleiman Mzee Chaaras ameipongeza Serikali ya CCM kwa juhudi iliyochukuwa na Utekelezaji huo wa Ilani ya CCM.
Nd. Suleiman alisema miradi mbali mbali ya Kiuchumi na Kijamii iliyoanzishwa ndani ya kipindi hichi cha Miaka Mitatu imewezesha kuleta tija kwa Maendeleo  na Ustawi wa Wananchi.
Wajumbe wa Kikao hicho Maalum wameiomba Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kuweka utaratibu mahsusi wa kuwapatia Mafunzo kama hayo kwa vile yameonyesha muelekeo wa kuwapatia Taarifa sahihi.
Kikao hicho kimetayarishwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ikiwa ni muendelezo wa kutoa Taarifa za Utekelezaji wa Ilani kwa Wananchi wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.