Habari za Punde

Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Gaudensia Kabaka Azungumza na Wazee wa Sebleni Akiwa Katika Ziara Yake Zanzibar.

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Gaudensia Kabaka  akizungumza na wazee pamoja na viongozi wa UWT Wilaya ya Amani ikiwa ni miongoni mwa muendelezo ya ziara yake Zanzibar (Kushoto) ni Katibu wa Umoja wa Wanawake Taifa Queen Mlozi na (kulia) ni Makamo Mwenyekiti U moja wa Wanawake UWT Taifa.
 Baadhi ya Wazee wanaoishi Sebleni wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT mama Gaudensia Kabaka.
Baadhi ya Wazee wanaoishi Sebleni wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT mama Gaudensia Kabaka.
Picha na Mwashungi Tahir wa Habari Maelezo Zanzibar. 
Na. Mwashungi. Tahir  - Maelezo Zanzibar. 14/03/2019.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Taifa UWT Gaudensia Kabaka ameipongeza Wizara ya Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto kwa kuwapo mafunzo ya ujasiriamali ya akinamama yenye lengo la  kuwakwamua na umasikini .
Hayo ameyasema leo huko katika ukumbi wa Sebleni wakati alipokuwa akizungumza na wazee pamoja na viongozi wa UWT Wilaya ya Amani ikiwa ni miongoni mwa muendelezo ya ziara yake Zanzibar.
Amesema Wizara hiyo ina haki ya kupongezwa kwa kuwakusanya akinamama na kuwawezesha kufanya kazi zao wenyewe na kuacha kujibweteka  kwa kujiongezea kipato  na kuacha  kuwasubiri akina baba.
Pia ametoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt Ali Mohamed Shein kwa kuendeleza na kuwathamini wazee kwa kuwapa matunzo mazuri ikiwemo pencheni kwa kila mwezi  na kuridhika katika maisha yao.
Aidha alisema wazee ni watu wa kuthaminiwa katika jamii na wao wana mchango mkubwa katika jamii familia   na wanataka matunzo  ndipo baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Rais wa kwanza  aliwajengea nyumba za makaazi kwa lengo la kuwataka waishi kwa amani na  utulivu.
“Tuwathamini wazee wanapokuwepo wanakuwa wana upendo na tunapata mambo mengi kutoka kwao ikiwemo busara, fikra na upendo “, alisema mama Kabaka.
Mama Kabaka aliwazawadia wazee hao zawadi mbali mbali ikiwemo sukari, mchele , mafuta ya kupikia , unga wa ngano , sabuni , khanga kwa akinamama na saruni kwa akinababa na shillkingi laki moja kwa ajili ya matumizi yao madogo madogo.
Wakati huo huo Mama Kabaka alitembelea skuli ya maandalizi ilioko Shauri moyo Tarakatul Jadidy na kuwaomba walimu wa kituo hicho wawe na subira kwani kufundisha watoto wadogo ni kazi kubwa aliwaomba wawe na subira na mungu atawalipa fungu lao.
Nae Katibu wa Wilaya ya Amani Asha Mzee akitoa taarifa fupi kwa kuwaomba viongozi wa majimbo kwa kuwa karibu na vijana na kuwapa mtaji kwa kuwapa elimu ili waweze kupata ajira au waweze kujiajiri wenyewe.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa inamalizika leo (jana Alhamis) kwa kukagua Tawi la Makadara lilioko miti ulaya na kutembelea kanisa la  Mkunazini na kufanya Mkutano wa ndani Amani Mkoa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.