Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Aweka Jiwe la Msingi la Sekondari ya Kardinali Pengo Ikwiriri

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wa pili kulia ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Fancis wa Asiz Ikwiriri, Padre Disma Kimboi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa ambaye alipewa nafasi ya kusalimia wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani Rufiji, Machi 29, 2019.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na wa nne kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani na  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri  mkoani Pwani, Machi 29, 2019.  Wengine kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francis wa Asiz Ikwiriri, Padre Dismas Kimboi
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya wasichana ya  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi  baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani,

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.