Habari za Punde

Halmashauri ya Wilaya ya Kati yasimamia zoezi la uchangiaji damu yavuna Lita 400 za damu

 Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya kati hasa wanawake ambao walijitokeza kwa wingi wakiwa katika viwanja vya Dunga walipoitikia mwito wa kuchangia damu kwa ajili ya benki ya damu na pia kuondokana na ile dhana kwamba mwanamke hachangii damu
  Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya kati wakiwa katika viwanja vya Dunga walipoitikia mwito wa kuchangia damu kwa ajili ya benki ya damu wakisajiliwa majina yao Vikosi vya ulinzi na usalama navyo havikuwa nyuma kwani navyo vilishiriki kwa kiasi kikubwa katika zoezi la kuchangia damu kwa jili ya Benki ya damu. Pichani wapiganaji kutoka vikosi vya JKU
Wachangiaji 300 wa mwanzo kila mmoja alizawadiwa  mwamvuli , Fulana pamoja na Vocha ya simu 
 Baadhi ya wananchi wakiendelea kutoa damu kwenye zoezi la kutoa damu lililoandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya katgi na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Bi Hamida Mussa Khamis
Baadhi ya wananchi wakiendelea kutoa damu kwenye zoezi la kutoa damu lililosimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya katgi na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Bi Hamida Mussa Khamis. Jumla ya lita 400 za damu zilipatikana na Wilaya ya kati hadi sasa inaongoza kwa katika uchangiaji wa damu.
 Mkuu wa Wilaya ya Kati Bi Hamida Mussa Khamis akizungumza na wapiganaji wa vikosi vya JKU mara baada ya kumaliza kujitolea kuchangia damu kaatika zoezi lililofanyika huko Dunga hivi leo
 Mkuu wa Wilaya ya Kati Bi Hamida Mussa Khamis akipata picha ya kumbukumu na wapiganaji wa vikosi vya JKU mara baada ya kumaliza kujitolea kuchangia damu katika zoezi lililofanyika huko Dunga hivi leo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.