Habari za Punde

Wananchi watakiwa kuthamini na kudumisha muungano

Mkoa wa Kaskazini Unguja.            
Wananchi wametakiwa kuenzi, kuthamini na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuendeleza Amani na kupata maendeleo.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi wakati walipofanya ziara na Ujumbe wa Watu 85 kutoka Kata ya Mbagala kuu Jijini Dar-es-salam,ziara ambayo imefanyika katika Hifadhi ya Samaki Fukuchani,Ujenzi wa Maskani ya Tushikamane Nungwi na Kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeleta mafanikio katika nyanja mbalimbali kama vile kielimu,kiuchumi na kukuza uhusiano mwema.
Aidha amesema Viongozi hao wametumia busara na hekima katika kuunganisha nchi mbili hizi ili kuweza kuwaletea maendeleo Wananchi wake hivyo ni vyema kuungana katika kuendeleza mambo mazuri walioyaanzisha.
Hata hivyo amewataka Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar kuhakikisha wanaulinda na kuudumisha Muungano huo kwa  nguvu zote kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mbagala kuu Khamis Shaaban Malenda amesema ushirikiano waliouanzisha Wadi ya Sogea na Kata ya Mbagala kuu utaweza kusaidia kupata mbinu za kubuni vianzio vya Mapato na kukuza uchumi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.