Habari za Punde

Mchezo wa Bonaza la Pasaka Kati ya Timu ya Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam Uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's Timu ya Ikulu Zanzibar Imeshinda Mchezo huo kwa Bao 6-2.

Kikosi cha Timu ya Ikulu Zanzibar kilichotowa kipigi kwa Timu ya Ikulu Dar es Salaam katika mchezo wa Tamasha la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar leo, Timu ya Ikulu Zanzibar imeibuka kwa ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya wageni wao. Tamasha laPasaka mwaka huu limefanyika Zanzibar na kujumuisha Timu mbalimbali rafiki kutoka Tanzania Bara kuadhimisha michezo mbalimbali katika viwanja tafauti vya Unguja.    
Wachezaji wa Timu ya Ikulu Sports Club ya Dar es Salaam na Ikulu Sports Club ya Zanzibar zikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza mchezo wao wa Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's leo kuadhimisha michezo hiyo hufanyika kila mwaka kwa kupisha katika pande hizo mbili za Muungano wa Tanzania. mwaka huu zimefanyika Zanzibar
Kikosi cha Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam kilichoshiriki mchezo wa Bonaza la Pasaka uliofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar na kukubali kichapo cha bao 6-2 dhidi ya ndugu zao Ikulu Sports Club Zanzibar, wakati wa kusherehekea michezo ya Pasaka Zanzibar kwa mwaka huu yamefanyika Visiwani Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg Salum Kassim Ali akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Ikulu Sports Club Dar es Salaam kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa Bonaza la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar.
Wanamichezo wa Timu ya Ikulu Zanzibar na Ikulu Dar es Salaam wakifuatilia mchezo huo wa Kirafiki wa Bonaza la Pasaka uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's, Timu ya Ikulu Zanzibar imeshinda bao 6-2. 














No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.