Habari za Punde

Mchezo wa Fainali ya Kombe la Muungano Kati ya Jangombe Boys na Pan African Itakayofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Kesho.26/4/2019.

Na Mwajuma Juma
FAINALI ya kombe la Muungano kwa mchezo wa mpira wa miguu inatarajiwa kupigwa kesho Ijumaa mjini hapa.

Fainali hiyo ambayo itawakutanisha Kati ya mabingwa watetezi wa kombe  Jang'ombe Boys ya Zanzibar na Pan African mabingwa wa Mkoa wa Dar Es Salaam itachezwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani hapa.

Katibu Kamati ya mashindano hayo hapa Zanzibar Kijo Nadir Nyoni alimwambia mwaandishi wa habari hizi kwamba maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yapo sawa na wanachosubiri ni timu kutoka dar ambayo itawasili Ijumaa yenyewe ya siku ya mchezo asubuhi na jioni watacheza mechi.

Alisema kuwa katika mchezo huo kiingilio ni shilingi elfu moja na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Diwani wa Kata ya Usaranga Kimara jijini Dar Es Salaam.

Alisema kuwa wanashukuru maandalizi yanaenda Kama walivyopanga na kutoa shukrani zao kwa kamishna wa michezo Sharifa Khamis kwa kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa Sana.

Awali kabla ya fainali hiyo walipanga kuchezwe mechi za mtoano ili kupatikane bingwa atakaecheza fainali hiyo lakini ilishindikana kutokana na ratiba ya uwanja na timu ambazo walizichukuwa zinabanwa na ratiba ya michezo yao.

Hivyo wameona ichezwe moja kwa moja fainali na timu bingwa mtetezi wa kombe hilo ambae ni Jang'ombe Boys.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.