Habari za Punde

RC Ayoub awataka Wananchi kuhudhuria kwa wingi maadhimisho ya kumuombea Marehemu Abeid Amani Karume

               Na Mwashungi Tahir      Maelezo    
            MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wananchi wa Mkoa huo kufika kwa wingi katika maadhimisho ya kumuombea dua  Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na viongozi wakuu na waasisi wa Mapinduzi waliokwisha kufika mbele ya haki kila      ifikapo tarehe 7-4. huko Kisiwandui.
Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa  ofisi yake ilioko Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya dua za viongozi hao wa kitaifa ambao waliitumikia nchi hii.
Amesema dua hiyo itayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali  Mohamed Shein itafanyika Kisiwandui na kuhudhuria viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kuwataka wananchi wahudhurie kwa wingii na kuwaomba  wawe watulivu .
Aidha Ayoub amewaomba wafanyabiashara na wenye vyombo vya moto kuwa wastahamilivu wakati wa dua hiyo kwa kufungwa njia itokayo michenzani hadi kisiwandui  mpaka itapomalizika dua hiyo hali itaendelea kama kawaida na iwapo watakuwa na matumizi ya njia watumie michenzani kupitia Maisara hadi Mkunazini.
Hata hivyo dua hiyo ilianza kwa kumuombea  Rais Mstaafu wa pili baada ya Mapinduzi al hajj Aboud Jumbe Mwinyi huko nyumbani kwake migombani nje kidogo ya mji, marehemu Katibu wa mwanzo wa Afro Shirazi Party mzee Thabit kombo .
Pia dua hiyo iliendelea kwa Marehemu Waziri Kiongozi mstaafu Dkt Omar Ali Juma huko kwao Wawi Pemba  na marehemu Rais Mstaafu Sheikh Idrissa Abdul Wakil iliofanyika kijijini kwao makunduchi.
Aidha aliwaomba wananchi wote kuwaombea dua viongozi hao kwani wao ndio waliotangulia kuiweka nchi katika hali ya amani hadi kufika sasa tuko huru na hatuna wasiwasi akiwemo Marehemu Mzee Abeid Karume.
Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi katika  Mkoa  wa  Mjini Magharibi Thobias Gesauda Sodeeka       ametoa tahadhari kwa wananchi kwenye suala la usalama amesema wamejipanga kila sehemu kuimarisha ulinzi.
Akitoa wito kwa wazazi kuwashughulikia vyema watoto ili wasije wakapotea na kuwataka wananchi wote wawe watulivu katika dua hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.