Habari za Punde

Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa haki kwa aliyetimiza masharti ya kuandikishwa

Na Masanja Mabula -Pemba
MSIMAMIZI  wa tume ya uchaguzi wilaya ya wete  Omar zubeir Mbwana amesema Tume ya uchaguzi imeandaa mikakati madhubuti ili kuhakikisha kila mwananchi aliyetimiza masharti ya kuandikishwa anapatiwa haki yake.
Amesema lengo la tume ni kuona vijana waliotimiza umri wa  miaka 18, wanaandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wanafunzi wa skuli ya Sekondari Mitiulaya kwenye zoezi la uhamaishaaji wa maandalizi ya mabaoresho ya daftari la kudumu la wapiga kura.
“Tume imeandaa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura, hivyo mikakati ya tume ni kuona kuwa mwenye sifa za kuandikishwa ataandikishwa kwenye daftari hilo”alisema.
Aidha amewataka wanafunzi kuhakikisha kwamba elimu waliyopewa wanaifikisha kwa jamii inayowazunguka ili iwe chachu ya kufanikisha maboresho ya daftari wakati ukifika.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa skuli hiyo Riziki Makame Faki ameipongeza tume ya uchaguzi kwa uwamuzi wake wa kutoa taalum kwa wanafunzi na kusema kuwa itasaidia kuufikisha ujumbe kwa walengwa.
Aidha Riziki ameahidi kwamba walimu wataandaa utaratibu wa kuwakumbusha wanafunzi juu ya zoezi la kuandikisha mara kwa mara ili kuwaweka tayari kushiriki.
“Hii taaluma imekuja wakati muafaka, na tunaahidi kuendelea kuwakumbusha wanafunzi ili wakati ukifika wawe tayari kushiriki kwa wenye sifa”alifahamisha.
Baadhi ya wanafunzi wamesema kupitia taaluma wlaiyopatiwa na Tume ya Uchaguzi wataifikisha kwa jamii inayowazunguka, na kuongeza kwamba itawaweka tayari kwa ajili ya kuandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Skuli nyengine zilizopatiwa elimu hiyo ni pamoja na Skuli ya Mchangamdogo ,Shengejuu na skuli ya Chasasa.
Zoezi hilo la utoaji elimu maskulini  ni miongonoi mwa zoezi la kuhamasisha wananchi wenye sifa za kujiandikisha na wale ambao wameshajiandikisha kwenda kuhakiki taarifa zao katika kuelekea mchakato mzima wa uandikishaji wa daftari la kudumu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.