Habari za Punde

Wakusanyaji wa taarifa juu ya maandalizi ya Mitaala mipya wartakuwa kushirikiana

 Washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji maoni juu ya mitaala mipya wakiwa katika majadiliano wakati waliposhiriki mafunzo ya mitaala
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji maoni wakisikiliza kwa makini
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Zanzibar Mwalim Suleiman Yahya akizungumza wakati akifungua mafunzo ya ukusanyaji maoni juu ya mitaala

MKURUGENZI wa Taasisi ya Elimu Zanzibar Mwalim Suleiman Yahya Amewataka wakusanyaji wa taarifa juu ya maandalizi ya Mitaala mipya ya Skuli za Maandalizi na Msingi kuwa na mashirikiano ya pamoja wakati wa ukusanyaji wa maoni ili waweze kukusanya taarifa zenye uhakika zitakazosaidia katika maendeleo ya elimu.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya ukusanyaji wa maoni juu ya mitaala hiyo katika kituo cha Walimu (TC), Kiembesamaki amesema hatua hiyo itaweza kusaidia upatikanaji wa taarifa ambazo zitajenga muelekeo mzuri ambao utamuandaa mtoto katika msingi bora wa kielimu.

Aidha Mkurugenzi huyo amewataka wadau mbali mbali kutoa maoni yao ili kuingizwa katika mtaala huo ikiwemo masuala ya rushwa na usalama barabarani ambayo yatawasaidia wanafunzi kuwa na uwelewa juu ya masuala hayo.

Akizungumzia suala la mashirikiano kwa jamii amesema mchakato huo utasaidia kuondosha malalamiko kwa wananchi juu ya kuwepo wingi wa masomo kwa wanafunzi wa Maandalizi na Msingi, hivyo amesema maoni yao ni muhimu na yatasaidia kupata mitaala bora.

Kwa upande wake mshauri muelekezi kutoka kampuni binafsi ya Elimu ya Dar-es-salam amewataka washiriki kukutana na walengwa wa mitaala ikiwemo walimu na wanafunzi kwani wao ndio wataweza kutoa maoni yaliyo bora yatakayojenga mustakali mzuri kwa wanafunzi pamoja na taifa.

Nao washiriki wa mafunzo hayo kutoka Unguja na Pemba wamesema watahakikisha wanatumia vizuri fursa hiyo waliyoipata kwa kuweza kuwafikia walengwa ili lengo la kuwapunguzia mzigo wa masomo wanafunzi hao liweze kufikiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.