Habari za Punde

Wazee wanahitaji kuthaminiwa

Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe Ramadhani Hamza Chande amesema Serikali imeweka Mikakati madhubuti ya kuhakikisha Wazee wanaishi katika mazingira mazuri na kuepukana na hali tegemezi.
Ameyasema hayo huko Tawi la CCM Matarumbeta wakati alipokuwa katika kikao cha kujadili matatizo yanayowakabili Wazee wa Shehia ya Jangombe na Matarumbeta na kuweza kuyapatia ufumbuzi.
Amesema amesema miongoni mwa matatizo yanayowakabili Wazee hao ni pamoja na Maradhi,Umasikini na baadhi yao kutengwa na familia.
Amefahamisha kuwa Uongozi wa Jimbo unafanya juhudi za kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili na yaliokinyume na uwezo wao watayafikisha Serikalini ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo amewaomba Viongozi wa Taasisis zinazohusiana Wazee kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanasimamia Wazee na kukakikisha wanapata haki zao za msingi.
Kwa upande wake Diwani wa Wadi ya Kwaalinatu Fatma Suleiman Juma amesema lengo la kuundwa Jumuiya hiyo ni kutetea maslahi ya Wazee bila ubaguzi wa Rangi,Dini na Siasa na kuwaomba Wazee hao kutumia Busara na Hekima katika kuiendesha ili malengo yao waweze kufikiwa.
Nao baadhi ya Wazee wa Baraza la Wazee Shehi ya Jangombe na Kwaalinato wamesema juhudi zinzazochukuliwa na Viongozi wao ni kubwa nab ado zinahitaji kuendelezwa kwa faida ya wazee wasasa na kipindi kijacho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.