Habari za Punde

Walimu Madrasah watakiwa kujisajili na kufuata mtaala wa aina moja

Walimu wa Madrasa za Qur-an Zanzibar wametakiwa kujisajili na kufundisha kwa kufuata Mtaala wa aina moja ili kuondosha usumbufu kwa Wanafunzi wao.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maandalizi na Msingi Safia Ali Rijali wakati alipokuwa akizungumza na ZBC huko Afisini kwake Mazizini Wilaya ya Mjini.
Amesema iwapo watasomesha kwa kufuata Mitaala ya pamoja kutaondosha tatizo la baadhi ya Wanafunzi kusomeshwa mambo mengi ambayo yapo kinyume na umri wao.
Aikielezea kuhusu ufungaji wa Madrasa amesema haipendezi hata kidogo kuona Madrasa nyengine zimefuingwa na nyengine zikiendelea kutoa elimu hivyo amewashauri kuweka mfumo mmoja wa kufunga na kufunguwa madrasa zao ili kuwaondoshea usumbufu Wanafunzi.
Aidha ameamewaomba Wamiliki na Viongozi wa Madrasa kuzisajili kupitia Ofisi ya Mufti ili ziweze kupatiwa Miongozo ya ufundishaji na fursa za Mafunzo zinazotolewa.
Hata hivyo amesikitishwa na baadhi ya Vijana wanaojiunga na vikundi vyenye Mnasaba na Dini na badala yake kuenda kinyume na miongozi,Misingi na Maadili ya vikundi hivyo kwa kufanya vitendo vya Udhalilishaji.
Mali na hayo Bi Safia amewashauri Wakuu wa Madrsa kuanzisha umoja wao ili waweze kukaa pamoja na kujadili matatizo yanayowakabili na kuayapatia ufumbuzi kwa haraka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.