Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ndugu Moh’d Nassor Salim akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la kujitolea la Nigeria-Technical Aid Corps (TAC) katika Ukumbi wa ofisi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Chake chake Pemba.
Ujumbe kutoka Shirika la kujitolea la Nigeria-Technical Aid Corps (TAC). (Kulia) niAdamu Jibirillaambae ni Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini na (kushoto) ni Hammawa Bunuyaminu Ofisa wa Mradi.
Walimu wanaojitolea kutoka Nchini Naigeria wakiwa katika
Ukumbi wa ofisi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Chake chake Pemba.
Na Ali Othman Ali
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Ndugu
Moh’d Nassor Salim amesema kupanda kwa kiwango cha ufaulu Kisiwani Pemba
kumechangiwa na juhudi zinazofanywa na
Shirika la kujitolea la Nigeria kwa kuleta walimu wa Masomo ya Sayansi.
Akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la kujitolea la
Nigeria-Technical Aid Corps (TAC) pamoja na walimu 16 wanaojitolea kutoka
Nchini Naigeria katika Ukumbi wa ofisiya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Chake chake Pemba Bw. Salim amesema kiwango cha ufaulu Kisiwani Pemba kimepanda
kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mkuu wa Shirika la Kujitolea la Nigeria Bw. Adamu Jibirilla
akielezea shukran zake za dhati kwa uongozi wa Wizara ya Elimu kwa mashirikiano
makubwa waliyoyapata amewataka walimu hao kundelea kufanya kazi kwa bidii na
kuwatabahisha kwamba huduma zao ni zenye kukubalika kisiwani Pemba.
Aidha Bw. Jibirillaamewataka walimu hao kuitumia vyeme fursa
ya kuwepo kisiwani Pemba kwa kujifunza lugha ya Kiswahili ambayo ameitaja kua
ni lugha inayozidi kujipatia umaarufu katika bara la Afika na Ulimwenguni kote.
Kwaupande wao walimu hao wakujitolea walipata fursa ya
kuelezea mafanikio na changamoto mbali mbali zinazowakabili, ambapo mwalimu
Yahaya Otori Muhammed anaefundisha Skuli ya Utaani ameliomba Shirika la
kujitolea la Nigeria-Technical Aid Corps (TAC) kukubali maombi ya kuleta walimu
wengine kujitolea katika Skuli za Zanzibar.
Nae mwalimu Bernard Augbedion anaejitolea katika Skuli ya
Ukunjwi, alimuomba Mkuu wa Shirika la hilo Bw. Adamu Jibirilla, kuzingatia
swala la jinsia wanapoleta walimu kisiwani Pemba ambapo alisema kwenye mwanaume
mwenye mafanikio lazima kuna mwanamke nyuma yake.
Jumla ya walimu 16 kutoka Nigeria (wote wanaume) wanafundisha
Skuli mbali mbali za Sekondari kisiwani Pemba.
No comments:
Post a Comment