Habari za Punde

Wakutubi, Watunza Nyaraka na Makumbusho Wametakiwa Kuelimisha Jamii Kupenda Kutembelea Sehemu za Makumbusho.

Na Mwashungi Tahir  Maelezo.
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud  aliitaka jumuiya ya Wakutubi , Watunza Nyaraka  na Makumbusho Zanzibar (AZLIS) kuelimisha jamii kupenda kufika  sehemu hizo kuwa na uelewa wa kusoma vitabu  na kutunza kumbu kumbu.
Akizungumza na wanajumuiya leo huko katika ukumbi wa Vyuo vya amali Rahaleo wakati alipokuwa akifunguwa mkutano wa pili  wa Jumuiya hiyo kuhusu umuhimu wake katika jamii juu ya kupenda kushiriki kupata kumbu kumbu na kuweza kuelimika.
Alisema jumuiya hii ya wakutubi , watunza nyaraka na Makumbusho Zanzibar ni muhimu sana kwa jamii na Serikali kwani  kusoma vitabu, kujua kumbu kumbu au nyaraka  ikiwemo ya nchi itakuwezesha weye   kupaswa kuhifadhi mambo yote muhimu yanayotokea katika jamii .
Alieleza kuwa asasi za kiraia ilojikita kwenye masuala  ya kumbu kumbu inaweza kusaidia sera ya elimu inaelekeza nyenzo muhimu ikiwemo maktaba wanafunzi kujisomea vitabu na kuwa mchango mubwa Serikalini.
“Nawaomba wanafunzi na wnanchi wa kawaida kuwa na muamko wa kupata muda wa kwenda maktaba au sehemu za makubusho ili kuweza kujipatia elimu na kufahamu mambo 
mengi yaliyotokea nchini”, alisema Ayoub.
Hivyo alisema tunapaswa wote kuwa na utamaduni  kufika maktaba kupenda kujisomea vitabu kwani ukisoma tayari unatanua akili, mawazo na kuunganisha na yale ya mtunzi na kuweza kupata kitu chenye uelewa zaidi.
Aidha Ayoub alisema jumuiya hii in nafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kuwa na utamaduni huo kwani mahitaji yataongezeka , fursa za ajira zitapatikana hasa kwenye masuala ya utalii utaweza kutembeza wageni kwa uhakika baada ya kupata ulewe wa majengo ya kumbukumbu .
Pia alieleza Serikali inajuwa umuhimu wa kutunza kumbukumbu na wala haikukosea kuweka chuo cha utumishi wa Umma kwani kila kitu lazima kiandikwe,kitunzwe na kihifadhiwe  ili  kumbu kumbu zisipotee ziweze kutumika hadi vizazi vijavyo.
Ayoub aliahidi kutoa mchango mkubwa na kufanya kazi bega kwa bega na jumuiya hiyo katika kuimarisha fani ya ukutubi ,makumbusho kumbu kumbu na kutaka jamii ijitokeze 
kusome fani hizo kwani zina fursa nyingi.
Kwa upande wa changamoto zinazowakabili  jumuiya hiyo ni pamoja na ukosefu wa jengo rasmi ambapo amewaahidi kuwasaidia kutafuta sehemu ya kukodi kwa mwaka mmoja 
na atalipia  na kuwasaidia  badhi ya  vifaa ikiwemo viti na kompyuta.
Nae Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Salum Sleiman Salum alisema juuiya hiyo inaunganisha taaluma kwa kubadilishana mawazo na ujuzi na iko tayari kutoa muamko wa kutosha kwa jamii kutumia sehemu hizo ili kupata taarifa zilizo sahihi.
Akitoa wito kwa Taasisi za Umma , Mashirika na  Mawizara wakati umefika na kutaka kujenga majengo na kuweka michoro ya chumba cha kutunza kumbu kumbu .
Sambamba na hayo Katibu wa Jumuiya hiyo ya Wakutubi , Watunza Nyaraka na Makumbusha Zanzibar Mohamed Khamis Kombo akisoma dhamira , malengo na matarajio  alisema lengo kuu ya jumuiya hiyo ni kujikusaya kwa pamoja kada zote ili kubadilishna mawazo.
Vile vile na kuwataka watu kuwa na muamko wa kwenda sehemu husika kujisomea na kujua kumbu kumbu zinazotokea kwenye jamii  kwa ni muhimu.
Mkutano huo wa siku mbili ambao unawasilisha mada mbali mbali zikiwemo Maktaba, kumbu kumbu na nyaraka,akumbusho na uhifadhi wa magofu  , na ujumbe wa wa mwaka huu TUMIA MAARIFA KWA MASLAHI YA JAMII.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.