Habari za Punde

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM KATIKA SHEREHE ZA KUMWAPISHA RAIS WA MALAWI PROFESA ARTHUR MUTHARIKA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi,  Bw. Ben Botolo wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chileka uliopo Blantyre nchini Malawi kuwakilisha, Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019

Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na , Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Chileka uliopo Blantyre Malawi kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa  Arthur Peter Mutharika, 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika wakati Rais huyo alipohutubia baada ya  alipoapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais huyo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika wakati Rais huyo alipohutubia baada ya  alipoapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais huyo 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa zamani wa Malawi, Bakili Muluzi katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehudhuria sherehe za kumwapishwa Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika zilizofanyika jijini Blantyre.

Amehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzi, Blantyre. leo (Ijumaa, Mei 31, 2019) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza baada kuapishwa, Rais Mutharika aliwaahidi wananchi wa Malawi kuwa atawatumikia bila ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini au ukabila.

Pia alisisitiza kuwa hatavumilia kuona vyama vya siasa, madhehebu ya dini au mtu yeyoye anaanzisha vurugu kwa nia ya kuikwamisha Serikali.

Rais Mutharika alisema kuwa waliomchagua na wasiomchagua wote ni rafiki zake na amedhamiria kuwatumikia kwa moyo wa upendo na haki.

“Uchaguzi umekwisha mshindi amepatikana, hivyo mnapaswa kuiunga mkoano serikali iliyodhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Malawi.”

Alisema wananchi wa Malawi wameamua kumchagua Profesa Mutharika na Chama cha Democratic Progressive Party (DPP) hivyo lazima waheshimiwe.

Awali, Waziri Mkuu alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chileka alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo.

Viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na Balozi wa Tanzani nchini Malawi, Ben Mashiba na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Chembe Muntali.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi. Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini leo jioni.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

IJUMAA, MEI 31, 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.