Habari za Punde

WATAALAM WA SHERIA WAITAKA SHERIA MPYA YA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI NCHINI

Mtaalamu anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo,akifafanua masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi wakati wa  mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hivyo, Jijini Arusha
Mkurugenzi wa  Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, (Wa kwanza kulia) na Mwanasheria wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Godwill Benda pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Inspekta. William Mkamba, wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha 
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha
 Mwanasheria kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Wa kwanza kulia), Mhe. Verynice Kawiche, na Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mhe. Gilbert Ndeoruo, (katikati) pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Merick Luvinga, wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha

Mkurugenzi wa  Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, (walio kaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakati wa  mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Juni, 2019


Na. OWM, ARUSHA
Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri kutungwa kwa sheria mpya itakayohusika na  ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi ili kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo kutoweza kueeneza  magonjwa  kwa binadamu.
Sheria hiyo imeshauriwa kuzingatia dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu, lengo nikusaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa kuvichukua  vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kuvisafirisha na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, uliofanyika kwa siku tatu na kufungwa leo  tarehe 31 Juni, 2019, Jijini Arusha, kwa pamoja,  wataalam wa sekta za Afya  na wanasheria wa sekta hizo wamebainisha kuwa uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuimarisha usalama  na ulinzi kwa wanaohusika na shughuli za vimelea hivyo, mafunzo kwa wataalamu hao, miundo mbinu  ya maabara, pamoja na kuainisha orodha ya vimelea hivyo.
Wataalamu wa sekta za Afya walioshiriki mkutano huo, wamebainisha kuwa, sheria hiyo ni ya muhimu kwa kuzingatia kuwa, Dunia imekuwa na tishio kubwa la magonjwa ya kuambukiza yanayoweza kusambaa kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa kwa binadamu, mifugo, wanyama pori na kuleta uharibifu wa mazingira. Wamefafanua kuwa,  Tafiti zinabainisha kuwa kila mwaka huibuka magonjwa ambukizi mapya kati ya matano hadi Nane duniani. Hivyo inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, dunia itakuwa na magonjwa ambukizi mapya 30.

 Akiongea wakati wa akifunga mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe amebainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii ya watanzania yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko,  hivyo ushauri huo wa wanasheria na wataalam wa sekta hizo za afya  utaratibiwa kwa uhakika ili kuweza kuijenga jamii salama.
Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.