Habari za Punde

Waandishi wa Habari Watakiwa Kiripoti Habari za Kijamii

Na Hawa Ally, ZANZIBAR
WAANDISHI wa habari wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuripoti kesi za udhalilishaji wa kijinsia pindi zinapofikia ngazi za mahakama ili kuihabarisha jamii kinachoendelea juu ya kesi hizo.
Hayo yameelezwa na mwanasheria kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar  Mohmed Salehe ambae pia alikuwa mkufunzi katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya  mwenendo wa kesi  katika Mahakma yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa TAMWA huko Tunguu.
Alisema waandishi wa habari wananafasi kubwa katika kukabilisha na jamii juu ya kupata haki zao katika ngazi mahakama pale kesi zao zinapofia katika ngazi hizo kutokana na baadhi ya jamii kutokuwa na uwelewa juu mwenendo wa kesi hususani pale zinapoharishwa na kupangia tarehe nyingine.
“Baadhi ya jamii bado hawana uwelewa wa mwenendo wa kesi katika mahakama  na kupelekea hadi wengine kushindwa kuendeleza kesi zao mfano pale inapoharishwa kwa shahidi kutofika mahakamani au ushahidi kutokamilika  kwa hiyo waandishi wa habari mnatakiwa muelimishe jamii kuhusu swala hili.”lisema
Aidha alisema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakiibua matukio mengi katika jamii lakini changamoto waliyonayo kwa waandishi wengi kushindwa kutokuwa na ufatiliaji wa kesi hizo.
“Utakuta waandishi wanaibua  mambo mengi katika maswala haya ya udhalilishaji lakini si wafatiliaji wa kesi pindi zinapofika mahakamani, wanakuja wakati ule ule tu ambao kesi bado yamoto na kuishia njiani kushindwa kupata mwendelezo wake’’Alisema.
Nae  Meneja mtetezi  wa chama cha waandishi wa habari wanawake TMWA Zanzibar Haura  Shamte alisema Mradi huo wa miaka mitatu  wa Jukwaa la habari la kumaliza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ambao unatoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa online  juu ya maswala ya  mwenendo wa mashataka katika mahakama pamoja na udhalilishaji wa kijinsia pamoja na maswala ya haki za binaa damu.
Alisema wanamatumaini makubwa mwisho wa mradi huo kutakuwa namafanikio makubwa katika kupunguza vitendo vya udhalilishaji na jamii kuwa na mwamko katika kufatilia kesi zao mahkamani.
Alisema TAMWA kupitia mradi huo wataemdelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari hususani  online Network ili kushajiisha katika kufatilia kesi zinapokuwa mahakamani hadi zinapomalizika.
Awali akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Dk. Mzuri Issa Aliamesema mchango wa vyombo vya habari ni mkubwa katika kuripoti kesi za udhalilishaji

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.